Uwanja
wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2
Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa
muda wa siku 14 tu.
Wakaazi
wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live
bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo
inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo
ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja
vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. Uwanja huu umejengwa kwa
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.
No comments:
Post a Comment