Rais wa Chama cha Waendesha Baiskeli Tanzania, Godfrey Jacks
Muhagama, ambaye pia ni miongoni mwa waendesha baiskeli kwenye msafara huo
ulioanzia Mbeya akitoa maelezo ya namna shughuli hiyo ilivyofanikiwa.
Mwakilishi wa Norwegian Church Aid nchini Tanzania, Tale
Hungnes
akiwapongeza waendesha baiskeli mara baada ya kufika Dar es Salaam
wakitokea kwenye mpaka wa Malawi na Tanzania, Kasumulo Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Rashid Rutengwe akisaini madai ya haki ili kuweka
imani yake kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa
kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika desemba mwaka huu huko
Paris, Ufaransa.
Wanafunzi
wa shule za msingi Wambi na Nyamalala, James Lyimo (kulia) na Vannesa
Mgata wakionyesha mti waliokabidhiwa kwaajili ya kupanda katika shule
zao
Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia
akikabidhi mti kwa viongozi wa dini Mufindi, Mkoani Iringa, kutoka kulia
ni Imamu wa Msikiti Mkuu wa Mafinga na Mch. Annuai Mwinuka wa KKKT,
Jimbo la Mufindi Usharika wa Mafinga, zoezi hilo lililofanyika kwenye
shule za Msingi Wambi na Nyamalala zote za Mafinga.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dr. Rashid Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya waendesha baiskeli na viongozi wa msafara huo
Ofisa
Miradi
wa Norwegian Church Aid, Nizar Suleiman akitoa maelezo juu ya msafara
wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi, baada ya
kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwenye shule ya Sekondari Kola
Hill.
Waendesha baiskeli wakiwa katika eneo la Ruaha Mbuyuni
Mwakilishi wa Norwegian Church Aid nchini Tanzania, Tale
Hungnes akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha baiskeli, walipofika kwenye mji wa Ilula, Mkoani Iringa.
Baadhi
ya akina mama wa mji wa Makambako wakisikiliza kwa makini maelezo
kutoka kwa vijana wahamasishaji wa elimu ya mabadiliko ya tabianchi wa
YouthCAN Tanzania
Msafara wa waendesha baiskeli ukiingia kwenye mji wa Ilula Mkoani Iringa
Esther
Joshua ambaye ni mwanamke pekee kwenye msafara wa kuendesha baiskeli
kutoka Mbeya mpaka Arusha, hapa akiwa nje kidogo ya mji wa Mafinga
kuelekea Iringa Mjini.
Waendesha baiskeli wakielekea jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro, Muhongo Rweyemamu akipanda mti kwenye shule ya
Sekondari Kola Hill, Mkoani Morogoro ambayo ni sehemu ya kampeni hiyo
Na Dotto Kahindi
Msafara wa
Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa
baiskeli ambao ulianza Octoba 17 mwaka huu kwenye mpaka wa Tanzani na Malawi
umefika jinini Dar es Salaam ambako utasimama kupisha zoezi zima la uchaguzi mkuu kabla ya kuelekea Namanga Arusha.
Msafara
huo ambao umekuwa ukipata mapokezi makubwa kutoka kwa viongozi
mbalimbali wa serikali, dini na wananchi kwa ujumla, ukiwa Mkoani
Morogoro ulipata mapokezi makubwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rajab
Rutengwe.
Mkuu huyo wa
mkoa amewapongeza waendesha baiskeli na kuwaita ni mashujaa na mabalozi wazuri
wa kuhamasisha jamii kutunza mazingira
na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Msafara huo
ambao umeanzia Msumbiji kupitia Afrika Kusini Botswana, Zimbabwe, Zambia,
Malawi na sasa Tanzania, utafikia kilele chake mjini Nairobi Kenya mwezi
novemba mwaka huu.
Dr. Rutengwe
amesema kuwa jambo la kutunza mazingira ili kupunguza athari za mabadiliko ya
tabianchi ni muhimu na ni jambo la kila mmoja wetu.
Amewakemea
viongozi wa serikali wanaoshirikiana na wananchi kuharibu mazingira kwa kukata
miti na kuuza mikaa na kuahidi kuwashughulikia baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.
Akizungumzia
umuhimu wa milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru anasema ni muhimu kwa kuwa ni
moja ya vyanzo vya maji ambayo huwanufaisha watu wa mikoa ya Morogoro, Dodoma,
Pwani na Dar es Salaam.
“Sisi watu
wa Morogoro tukiwa wabinafsi kwa kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya uharibifu
kwenye milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru tutakuwa tunawaua wenzetu
wanaotegemea milima hiyo” anasema Dr. Rutengwe
Akitoa
taarifa ya msafara huo, Ofisa Miradi wa Norwegian
Church Aid, Nizar Suleiman anasema kuwa lengo la msafara huo ni kujenga uelewa
kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupitia uendeshaji wa baiskeli na
kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini kufikisha elimu hiyo.
Anasema
msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka imani zao
kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa
mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika desemba mwaka huu huko Paris,
Ufaransa.
Msafara huo unatarajiwa
kuendelea tena novemba 3 mwaka huu, ukitokea jijini Dar es Salaam
kuelekea Namanga Mkoani Arusha ambapo utakabidhiwa kwa waendesha
baiskeli wa Kenya.
No comments:
Post a Comment