Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia),
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya
nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa
ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na
Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia),
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya
nchini India, Bhimasena Rau wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa
ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama
ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la
Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu
kushoto), akitoa neno la shukrani baada ya kusaini mkataba wa ununuzi wa
magari ya Kampuni ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Magari hayo ni kwa
ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Ofisi ya
Waziri Mkuu-TAMISEMI. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI, Jumanne Sagini, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili
kulia) akipokea Mkataba wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa
Jeshi la Magereza kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Ujenzi ya Poly
Technologies ya nchini China. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja. Halfa hiyo ilifanyika katika Ukumbi mdogo
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima
(katikati aliyevaa tai), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil (wakumi kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri
Mkuu-TAMISEMI, Jumanne Sagini (wanane kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa
Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
SERIKALI ya
Tanzania imeingia Mkataba wa ununuzi wa magari kwa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama nchini na Kampuni ya Motorrama (T) LTD ambayo ni Wakala wa
Magari aina ya ASHOK LEYLAND kutoka nchini India.
Mkataba
huo umesaniwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Job Masima pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo ya
Utengenezaji wa magari, Bhimasena Rau ukishuhudiwa na Wakuu wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada mkataba huo kusainiwa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja aliishukuru Serikali kwa msaada huo ambao
utasaidia kutatua tatizo la uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza.
“Utekelezaji
wa mpango huu katika Jeshi la Magereza utakuwa na manufaa makubwa kwani
utapunguza tatizo la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za
uendeshaji na utawala pamoja na utekelezaji wa jukumu la kuwasafirisha
Mahabusu kwenda mahakamani na kurudi magerezani,” alisema Minja.
Lengo
kubwa la ununuzi wa Magari hayo unalenga kuboresha huduma za usafiri
pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Vyombo vya
Ulinzi na Usalama hapa nchini.
No comments:
Post a Comment