Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mgeni
rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro
Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa.
Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
Mgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine
alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa
hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu
siku ya uchaguzi.
Mgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ofisi yake imepata taarifa
kuwa kuna baadhi ya wagombea wanatembea na silaha za
moto,mapanga,manati na kufundisha vijana mbinu za kuvunja amani siku ya
uchaguzi.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisisitiza kuwa watu wote
waliojiandikisha wana haki ya kupiga kura Oktoba 25,2015 na kuwataka
baadhi ya watu wanaojipanga kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura
kuachana na wazo hilo na badala yake waendelee tu shughuli zao na
wakati muda wa kutangazwa matokeo ndiyo warudi vituoni
Wadau
wa mkutano huo walisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kisha
kuendelea na shughuli zao Oktoba 25,2015 badala ya kukaa mita 200/300
kutoka kwenye kituo cha kupigia kura kwa vile kila chama kitakuwa na
wakala wake hao ndiyo wataweza kulinda kura zao .Kushoto ni kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Wadau
wakiwa ukumbini,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro.Wadau wa amani mkoani Shinyanga pia walikubaliana kukabiliana na
watu wote wanaopanga kuvuruga amani ya nchi wakati wa uchaguzi.
Mwakilishi wa shirika la Save the Children Herman Mbunda akizungumzia umuhimu wa kulinda watoto wakati huu wa uchaguzi
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'umbi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(kulia) 
Wadau
hao walikumbushana na kuhamasishana kulinda haki za watoto,wanawake na
makundi maalum katika jamii wakiwemo walemavu wakati wa uchaguzi
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao
hicho cha wadau wa amani walisema ni vyema katika kipindi hiki cha
uchaguzi kila jambo linalofanyika basi kuwe na maslahi kwa watoto ambao
asilimia kubwa wanaingizwa katika masuala ya siasa
Wadau wa amani wakiwa ukumbini
Katibu
wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pili
Misungwi(kushoto) akifuatilia kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri
ukumbini
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede(kulia)
Mkutano unaendelea
Kikao cha wadau kinaendelea
Mkutano unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Viongozi wa dini wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Kaimu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago(kulia)
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akiwasilisha mada ya
ulinzi na usalama katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 ambapo
alisisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na watu
watakaovuruga amani ya nchi
Kikao kinaendelea
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika kikao
hicho ambapo aliwataka waandishi wa habari nchini kutumia vizuri kalamu
zao ili kudumisha amani ya nchi
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Picha ya pamoja washiriki wa kikao hicho
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya kumbukumbu
Picha ya kumbukumbu. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment