Urembo : Balozi wa LuvTouch Manjano Atembelea Washiriki wa Semina ya Ujasiriamali - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 15 September 2015

Urembo : Balozi wa LuvTouch Manjano Atembelea Washiriki wa Semina ya Ujasiriamali

  
 


 Balozi wa Luv touch Manjano Irene Pul Katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Semina ya ujasiriamlai ya wanawake kwa kupitia Vipodozi vya Luv Touch manjano iliyochini ya Manjano foundation.

Lengo la Mradi huo ni kuona kwamba wanawake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi, yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia ujasiriamali.Balozi huyo amewashauri Washiri hao kwanza kupenda ujasiriamali na kufanya kazi kwa bidii lazima watafanikiwa.

Pili kila mshiriki kuwa mbunifu kwenye biashara na kuja na kitu cha kipekee ambacho kitawafanya watumiaji wa luv Toch manjano pamoja na wateja wengine kushawishika kuwaunga mKono washiriki hao katika biashara yao pamoja na kuwatangaza kwa watu wengine wengi zaidi. 
 Pamoja na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu (Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.

No comments:

Post a Comment