Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali
la READ International, Rob Wilson (katikati) akizungumza katikasherehe
za miaka 10 ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya
wanachama wa shirika hilo la kujitolea nchini Tanzania. READ
International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa ikisihirikiana na
Realising Education for Development pamoja na wahisani wengine imeweza
kusaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4
nchini kote.
Mjumbe wa Bodi ya READ International,
Faraja Kotta Nyalandu (kulia), mwanzilishi wa READ, Tom Wilson (wa pili
kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Makumbusho
ya jijini Dar es Salaam wakikata keki kusherehekea miaka 10 ya shirika
hilo.
Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali
la READ International, Rob Wilson (kulia) akizungumza na baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho alipotembelea maktaba ya
shule hiyo iliyowezeshwa kwa ufadhili wa shirika hilo kwa kushirikiana
na Realising Education for Developmentpamoja na wahisani wengine.
READ International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa huku ikisaidia
ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote.
Wengine pichani ni baadhi ya walimu wa shule hiyo.
Mmoja
wa wanachama wa kujitolea wa READ, Amani Alphonce Shayo akizungumza
katika hafla hiyo jinsi mpango wa ukarabati wa maktaba ulivyoleta
manufaa kwa wanafunzi wa kitanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya READ International, Hatima Karimjee akizungumza katika sherehe za miaka 10 ya shirika hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya
MANTRA, Frederick Kibodya akizungumza kuhusu ufadhili wao katika katika
kuisaidia READ International kwa ushirikiano na Realising Education for
Development katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyenzo za elimu
katika shule za sekondari nchini.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho ya jijini Dar es Salaam
wakijisomea katika maktaba iliyowezeshwa na Shirika la READ
International kwa kushirikiana na Realising Education for Development. READ
International imetimiza miaka 10 tokea kuanzishwa ikisaidia ujenzi wa
maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote.
ILI kukabiliana na tatizo la miundombinu katika sekta
ya elimu nchini inayozikabili shule nyingi sa sekondari, Shirika lisilo la Kiserikali la READ
International kwa kushirikiana na mpango wa Realising Education for Development
limetangaza mpango wa kujenga zaidi ya maktaba 500 katika kipindi cha miaka 10
ijayo ili kuinua kiwango cha elimu nchini.
Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10
tokea kuanzishwa kwa shirika hilo, Muasisi wake Rob Wilson alisema jijini Dar
es Salaam juzi kuwa kupitia michango ya wafadhili wao pamoja na Realising
Education for Development wanaweza
kujenga japo maktaba 50 kwa kila mwaka.
“Katika kipindi cha
miaka 10 tumefanikiwa kusidia vitabu milioni 1.4 na kujenga maktaba takrabani
72. Kwa msaada wa wadau wa elimu tumefika hapa, sasa tunakusudia kufanya vizuri
zaidi katika miaka 10 ijayo,” alisema bwana Wilson.
.
Muasisi huyo alisema wanajivunia mchango wanaoupata kutoka
kampuni mbalimbali na kuzitaja baadhi kama Bakhresa, Simba Cement, Wentworth,
Mantra, Atlas Copco, na Songas na kusema ni matumaini taasisi nyingine kwa
kuona mafanikio waliyoyapata watajitokeza na kuwaunga mkono.
“Ikiwa ni sehemu ya Mpango wa Ukarabati wa Maktaba wa READ
kwa kushirikiana na Realising
Education for Development na wanachama wa shirika hili wa kujitolea hugeuza
vyumba visivyotumika katika mashule na kuwa maktaba nzuri na kisha kuziwezesha
kwa nyenzo muhimu kama vitabu, meza, viti na makabati,” aliongeza muasisi huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa READ
International nchini, Montse Pejuan alisema
licha ya ujenzi huo wa maktaba lakini pia wamesaidia kufundisha wakutubi
na kusaidia shule kufundisha walimu wao
wa maktaba.
“Tunafanya bidii kujenga mpango mzuri utakaowawezesha
wanafunzi kupenda kujisomea na hivyo kuwawezesha kufaulu vizuri masomo yao,”
alisema.
Kwa upande wake msemaji wa Kampuni ya Simba Cement Bi.Mtanga
Noor alisema kampuni yao imetumia takribani shs milioni 48 kusaidia ujenzi wa
maktaba tatu jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa makampuni mengine kuisaidia
juhudi za READ ili kuleta mabadiliko katika ubora wa elimu nchini.
Mbali ya Simba Cement wadhamini wengine ni Hogan Lovells,
MeTL Group, Wizara ya Elimu na Mazunzo ya Ufundi, Radar Education Ltd, KPMG,
IMMMA Advocates, Nabaki Afrika, Oyster bay Group, Learning InSync, MANTRA,
Wentworth Foundation, Bakhresa Group, Songas, na BG
Tanzania.
Wengine ni
pamoja na Karimjee Jivanjee Foundation, Better World Books, Veolia, klabu za Rotary za Oysterbay
na Bahari, Bakhresa Group, Hogan Lovells,
Corona, Atlas Copco, Aidan
Publishing na APENET.
No comments:
Post a Comment