Mgombea Ubunge wa jimbo la Arumeru magharibi
Gibson ole Meiseyeki
Gibson ole Meiseyeki
Na Woinde Shizza,Arusha
wananchi hapa nchini wametakiwa kuacha masihara ya kutoa kura zao kwa
wananchi hapa nchini wametakiwa kuacha masihara ya kutoa kura zao kwa
kudanganya kwa kupewa sukari,pesa na khanga, vitambaa ili waweze
kuwapigia kura wanasiasa wanaowarubuni ili kuweza kupata nafasi za
uongozi kuanzia ngazi za uraisi,ubunge na udiwani kwani wanakuwa
wanapoteza haki zao.
Na endapo watatoa kura zao kwa kununuliwa na kutofanyiwa yale
wanayoahidiwa na kupewa moyo badala yake viongozi hao wakisiasa pindi
wapatapo nafasi hizo wanafanya yao na kuwaacha wananchi wakitaabika na
hali ngumu ya maisha yale yale ambayo yamepitiwa na chaguzi mbalimbali
na ahadi lukuki ambazo wanapewa na wagombea wa nafasi mbalimbali
badala yake wabadili mtazamo wao kwa kuchagua viongozi waukawa hususan
chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ili kuweza kuwaletea
mabadiliko ya kweli nayaharaka.
Hayo yameelezwa na mgombea Ubunge wa jimbo la Arumeru magharibi
Gibson ole Meiseyeki wakati akinadi sera zake kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika katika viwanja vya kijiji cha kiranyi iliyoko
kata ya kiranyi katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha na kuhudhuliwa
na maelfu ya wananchi katika viwanja hivyo.
Aidha ameongeza kuwa anaomba ridhaa kwa wananchi ili kuweza kumchagua
na kuenda kuikomboa nchi na mwananchi wakawaida ili kuweza kumudu
maisha ya hali ngumu ya sasa ili kuweza kuleta maendeleo kunazia ngazi
ya kitongoji ,kata ,tarafa hadi taifa kwa lengo l kumkomboa mwananchi
ili kuweza kujiletea maendeleo yake mwenyewe.
Hata hivyo alivitaji viapaumbele vyake kuwa nikuleta maendeleo katika
sekta ya elimu .miundombinu ya barabara ,sekta ya afya ,maji ili
kuweza kuikomboa nchi na wananchi wake walioko.
Aidha aliongeza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa hospitali katika kata
hiyo atawajengea na kuweza kujenga shule nzuri yenye ubora wa hali ya
juu ili kuweza kupambana na adui umaskini na maradhi na ujinga.
Sambamba na hilo atahakikisha anasimamia vyanzo vya mapato
vinaongezeka kwa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo ya haraka
katika jimbo hadi Taifa kwa kushirikiana na mh,Raisi wake Edward
Ngoyai Lowassa ikiwa nisehemu ajenda ya maendeleo ni sera ya chama na
umoja wao.
Aidha aliongeza kuwa ajenda ya elimu ni vipaaumbele cha kwanza hadi
tatu hali ambayo ukimpa mwananchi elimu anaweza kujikwamua na hali
halisi ya ,maisha magumu yaliyoko sasa ambapo wanashindwa kumudu hali
ngumu ilyoko sasa kwani chadema wamejipanga kweli kweli kuweza kuleta
mabadiliko ya kweli kuanzia ngazi ya uraisi ,ubunge na udiwani.
Awali akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Seneu aliwataka wanachi
kuchagua mafiga matatu (full suite)ili kuweza kuenda na kuleta
mabadiliko ili kuweza kutobakwa na vyama vingine kwa kuwa na viti
vingi katika kufanya na kuamua maamuzi mbalimbali ya maendeleo na
ajenda katika vikao mbalimbali katika halmashauri,bunge na mabaraza ya
mawaziri.
Aliwataka wapiga kura kuweza kutoogopa kufanya mabadiliko katika
nafasi za kisiasa ili kuweza kuletewa mabadiliko chanya na ya haraka
katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake mgombea udiwani Gibson ole Meiseyeki amewataka
wananchi kuweza kumchagua jembe ili kuweza kuwaondolea shida na
changamoto zilizoko katika kata yao kwani hakuna mtu anavumilia shida
na kupenda maisha magumu.
No comments:
Post a Comment