Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI
ya Tanzania imeelezea utayari wake wa kupiga jeki na kuwajumuisha
wafanyakazi wa afya ya jamii katika nguvukazi ya sekta ya afya (national
health workforce) ya taifa ili kuboresha afya ya jamii hususani katika
maeneo ya vijijini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa mradi wa mafunzo ya
wafanyakazi wa afya ya jamii (Community Health Worker Learning Agenda
Project - CHW-LAW) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji (idara ya
uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi
Georgina Msemo alisema ni muhimu kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya ya
jamii ili kukidhi mahitaji ya kijamii.
Akimwakilisha
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Dkt Neema
Rusibamayila, Msemo aliwaasa wadau kufanya tafiti ya kisayansi ili
kukabiliana na hali ya upungufu wa wafanyakazi wa afya ya jamii, ambao
umekuwa ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma za kiafya nchini.
Msemo
alipongeza hatua ya wadau hao kwa kuzungumzia masuala ya wafanyakazi wa
afya ya jamii pamoja na kuja na mradi utakaowezesha wafanyakazi hao
kupata mafunzo ya kila mara ili kuboresha utendaji wao katika utoaji wa
huduma ya afya ya jamii.
Alisema
wafanyakazi wa afya ya jamii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya
jamii ikiwa pia katika uboreshaji wa sekta ya afya haswa katika magonjwa
ya malaria, kifua kikuu, VVU/Ukimwi, afya ya Uzazi na mtoto.
Naye,
Profesa Japhet Killewo, ambaye ni Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya
wafanyakazi wa afya ya jamii, alisema lengo la semina hiyo ya siku nzima
iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
lilikuwa ni kuwakutanisha pamoja wadau katika afya ya jamii pamoja na
wahisani kujadili utekelezaji wa utafiti uliofanywa na njia bora za
kuiboresha na kuikuza sekta ya afya nchini.
Killewo
alisema kuwa wafanyakazi wa afya ya jamii wamekuwa kwa miaka mingi
wakikosa kutambuliwa kwa kuwa wengi wao walikuwa darasa la saba na
wahitimu wa kidato cha nne, wengi wao mbali ya kuwa na uzoefu, wamekuwa
wakifanya kazi za kuijtolea bila mshahara.
Alisema kuwa hilo limechangia kukosekana kwa jitihada madhubuti ya kazi miongoni mwao.
Alisema
kuwa na ndiyo sababu CHW-LAW, wakishirikiana na serikali na wahisani
ambao ni pamoja na USAID, Muhas na Johns Hopkins wameamua kuandaa semina
hiyo kwa wafanyakazi wa afya ya jamii.
Alisema
kuwa semina hiyo, ambayo pia itafanyika mwezi oktoba, itafanyika katika
mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Kigoma, Simiyu, Shinyanga na Tarime,
ambayo ipo katika mpango wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result
Now). Ambapo wapatao wafanyakazi 300 wa afya ya jamii wanatarajia
kuudhuria.
Alisema semina kama hizo zikipewa msukumo na serikali na wahisani mbali mbali pia zitafanyika katika mikoa mingine nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya
ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa Juu
Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar
es Salaam Jumanne.
Mchunguzi
Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, Profesa Japhet
Killewo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani)
wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo
kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
Mkurugenzi
Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya
ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa Juu
Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar
es Salaam Jumanne.
Mkurugenzi
Msaidizi, Ukuzaji Afya Bi Hellen Semu, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani)
wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa Juu Agenda ya Mradi wa
Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
Mwakilishi
kutoka United States Agency for International Development (USAID), Bi
Anna Bodipo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa Juu Agenda ya Mradi
wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam
Jumanne.
Wadau
wa sekta ya Afya ya Jamii katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa
semina ya Wadau wa Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa
Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. Picha na mpiga picha wetu.
No comments:
Post a Comment