Matukio : Mhe. Issa Usi Gavu Afungua Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, Mtwara - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 22 September 2015

Matukio : Mhe. Issa Usi Gavu Afungua Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, Mtwara


Sehemu  ya wajumbe wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara, wakisikiliza mada mbalimbali zinazohusu changamoto na mikakati ya kuboresha mazingira ya Usafiri wa Majini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, akitoa shukrani zake kwa Ushirikiano unaoonyeshwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya Uchukuzi kabla hajamkaribisha Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano kufungua rasmi  Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara.
 Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande, akifafanua jambo katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Kikosi cha Meli Vita (701 KJ), TPDF-NAVY, Brigedia Generali, Richard Makanzo, akifafanua jambo,  katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar, Issa Usi Gavu, akifungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara.Maadhimisho ya Siku ya Bahari yanafanyika Kitaifa Mkoani Mtwara kwa siku tatu. 
(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment