Mkimbizi
kutoka Burundi, Philipo Nyandungulu, akishuka kutoka kwenye basi baada
ya kuwasili katika kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Kasulu mkoani Kigoma. Idadi ya wakimbizi kutoka Burundi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika
la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHRC) imekuwa ikiwahifadhi kwa
muda katika kambi hiyo.
Baadhi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi, wanaohifadhiwa
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakiwapokea
wakimbizi wenzao (hawapo pichani) waliowasili jana kwa basi kwa ajili ya
kuhifadhiwa katika kambi hiyo.
Mkimbizi kutoka Burundi,Philipo Nyandugulu(kushoto) na mkewe Vanisi Nyandugulu, wakisubiri taratibu za kupangiwa sehemu ya
kuishi baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma, baada ya kuwasili katika kambi hiyo jana.
Mkimbizi kutoka Burundi, Vanisi Nyandugulu akipanga vifaa
vyake baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma jana. Wakimbizi
kutoka Burundi wanaendela kuwasili nchini ambapo wanahifadhiwa katika kambi ya
wakimizi ya Nyarugusu.
Koplo Flora Peter wa
Kituo cha Polisi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu akiwa ameshikilia visu,
panga na fimbo vilivyokutwa katika baadhi ya mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi
wanaowasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma. Vifaa vya hatari kama
vile visu, panga, fimbo na mishale haviruhusiwi kumilikiwa na wakimbizi wapya
wanaowasili kambini hapo, kwa sababu za kiusalama.
Mkimbizi kutoka Burundi, Nibaruja Europernce , akihamasisha wenzake
wanaowasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma kuhusu taratibu za kuishi kambini hapo ikiwani ni pamoja na
kutekeleza masuala muhimu ya kiafya, jana.
Mfanyakazi wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira (TWESA)
linalofanya shughuli zake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Andrea Niyitanga , Akimnawisha mikono kwa
kutumia maji yaliyowekwa dawa, mkimbizi kutoka Burundi ikiwa ni mojawapo ya
mkakati wa kutoa elimu ya afya.
Mtoto Olivia Nekwizera, ambaye ni mkimbizi kutoka Burundi
akisaidiwa na mama yake kunawa mikono baada
ya kuwasili katika kambi ya wakimizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma. Kunawa mikono kwa maji yenye dawa ni jambo la lazima kwa
wakimbizi wapya kuonyesha umuhimu wa kuzingatia masuala ya afya na pia
kudhibiti magonjwa ya kuambukiza.
Watoto wa moja ya familia ya wakimbizi kutoka Burundi
wakielekezwa kuingia katika makazi yao mara baada ya kuwasili katika kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Anayeelekeza ni mfanyakazi wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira (TWESA)
linalofanya shughuli zake katika kambi hiyo.
Wakimbizi kutoka Burundi wakipata maelezo ya jinsi ya kuishi
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma
mara baada ya kuwasili kambini hapo.
Anayetoa maelekezo hayo ni Nayiga Mireye wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira
(TWESA) linalofanya shughuli zake kambini hapo.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment