Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha mkoba wenye Fomu za kuwania nafasi
hiyo, leo Agosti 23, 2015, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha
akimkabidhi Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha
Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo
Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mgombea Urais wa
Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad, baada ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23,
2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani,
Zanzibar. Kulia kwake ni Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja
na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha
akisoma taarifa ya muongozo kwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA
kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa
kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi
wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Maalim Seif alisindikizwa na Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza, Dkt. Juma Haji Duni pamoja
na viongozi wengine wanaounda UKAWA
No comments:
Post a Comment