Meneja
Mkuu Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC),
Mhandisi Boniface Njombe (aliyesimama) akielimisha Umma wa Kata ya Swaya
wakati walipotembelea eneo la kata hiyo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya
uelimishaji kuhusu manufaa ya Jotoardhi hivi karibuni mkoani Mbeya.
Kushoto ni Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli
Mnjokava.
Mkurugenzi
wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava.(aliyesimama
mbele) akichangia mada kuhusu jotoardhi na manufaa yake kwa wakazi wa
Kata ya Swaya hivi karibuni mkoani Mbeya.
Baadhi
ya Wakazi wa Kata ya Swaya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Kampuni ya
Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi (TGDC) wakifuatilia uwasilishwaji wa
mada toka kwa Meneja Mkuu wa TGDC hivi karibuni mkoani Mbeya.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Mbeya.
Mkoa
wa Mbeya unasemekana kuwa ni moja ya maeneo yaliyobarikiwa kuwa miongoni
mwa maeneo ambayo Shirika la Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC)
linatarajia kuanza shughuli ya uchimbaji jotoardhi kutokana na tafiti za
awali kuhusu nishati hiyo kuanza katika mkoa huo.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe wakati
wa Kampeni ya Uelimishaji kuhusu Jotoardhi kwa viongozi katika ngazi za
Kata za Ilomba katika Vijiji vya Ituha, Tonya pamoja na Kata nyingine ya
Nanyala iliyoko Mbozi Mkoani Mbeya.
Mhandisi
Njombe amesema kuwa, TGDC ina malengo ya kuzalisha zaidi ya megawati
200 kwa mkoa huo licha ya mkoa huo kwa sasa kutumia megawati 40 jambo
ambalo linaweza kupelekea nishati hiyo itakayozalishwa kupeleka katika
mikoa mingine ya jirani kwani kiasi hiko cha umeme kitakuwa ni kikubwa.
Aidha,
amewataka wakazi wa Mbeya kuonyesha ushirikiano kati ya Serikali yao
pamojana TGDC ili zoezi hilo lenye manufaa kwao liweze kufikiwa kwa
maendeleo ya mkoa na vijijini ambako kuna changamoto ya ukosefu wa
nishati ya umeme pia kutatua tatizo la mgao wa umeme katika mkoa huo.
“Tuunge
mkono jitihada hizi za Serikali ili walau nishati hii izidi kuendelezwa
na ituokoe dhidi ya hali ya umeme isiyokuwa na uhakika kwani
tukishakuwa na uelewa na kuelimisha wananchi na kutoa ushirikiano,
tutakaa mkao wa kula kutokana na nishati hii”, alisema Njombe.
Kwa
upande wake Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Bwana Jacob Mayalla ameeleza kuwa kutokana na juhudi za Serikali, tafiti
za jotoardhi nchini zilizanza miaka ya 1976 hadi mwaka 1978 zikiwa kama
tafiti za awali ambazo ziliweza kubainisha maeneo katika nchi ya
Tanzania kwenye maeneo yaliyopitiwa na Bonde la Ufa ambapo viashiria vya
jotoardhi vipo.
“Kwa
Mkoa wa Mbeya, tafiti za jotoardhi zilifanywa na Serikali kwa
kushirikiana na Wakala wa Jiolojia Tanzania”, alisema Mayalla.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Kiufundi toka Kampuni ya TGDC, Bwana
Taramaeli Mnjokava ameyataja baadhi ya matumizi ya moja kwa moja ya
jotoardhi nchini ikiwemo matumizi ya kiutalii ambapo maji ya jotoardhi
huwekwa kwenye mabwawa hivyo huvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kwa
kuyaoga na kuyaangalia jambo ambalo linaongeza pato la taifa.
Aliongeza
kuwa, maji ya jotoardhi hufaa kwa matumizi ya uzalishaji wa samaki
kwani samaki hupenda maji yenye hali ya uvuguvugu kuliko yenye baridi
hasa kwa maeneo yenye baridi kama mkoa wa Mbeya, hivyo pindi mabwawa ya
samaki yanapotengenezwa na kuwekewa maji ya jotoardhi yanasaidia
kuzalisha samaki kwa wingi jambo ambalo nalo litakuza pato kwa taifa na
kwa eneo husika ambalo uzalishaji unafanyika.
“Maji
ya jotoardhi yanaweza kutumika katika uzalishaji wa mboga mboga au maua
kwa njia ya Vitalu Nyumba kwa Kiingereza huitwa Green Houses lakini ni
vitalu hutengenzwa kwa plastiki au kioo, hivyo watu hutumia vitalu hivi
jambo ambalo linavutia sana soko la nje kwani huwa hawapendi mboga
zilizopigwa dawa wala maua yaliyopigwa dawa, niwahamasishe kujiandaa kwa
kuupokea mradi huu kwani utawanufaisha vyakutosha nyie wakazi wa Mbeya
na taifa kwa ujumla,” alisema Mnjokava.
Mnamo
tarehe 19 Disemba, 2013 Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ugavi wa
Umeme (TANESCO) ilisajiri kampuni ya kuendeleza nishati itokanayo na
Jotoardhi, jina la kampuni likiitwa “Tanzania Geothermal Development
Company Limited (TGDC).
Kampuni
hii ilianzishwa kama kampuni tanzu ya Shirika la TANESCO ambalo
linamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na mnamo mwezi Julai 2014 TGDC
ilianza kazi zake rasmi ikipewa jukumu la kuharakisha uendelezaji wa
nishati ya jotoardhi nchini.
No comments:
Post a Comment