Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda Akiwa na
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius
Magabe Tayari kwa Uzinduzi wa Kampuni ya Sanlan.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda wa Pili Kushoto
Akiwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance
Ndg.Julius Magabe, wa pili kulia Pamoja na
Mtendaji
Mkuu wa umoja wa makampuni ya Sanlam.Ndugu.Ian Kirk..Israel Kamuzora,
Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Mara baada
Uzinduzi wa wa Kampuni ya Sanlan wakionyesha Mshikamano.
Kampuni inayoongoza katika bima za maisha nchini, African life .
Assurance(Aflife) usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.
Assurance(Aflife) usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.
Kwa
mujibu wa Bw Magabe, Sanlam Group ni kampuni ya kuheshimiwa Afrika
yenye matawi katika nchi 12. "Kwenye suala la wateja kuridhika na
uaminifu, Sanlam imekuwa ikiipa sekta ya bima ya maisha kipaumbele kwa
wakazi wa Afrika Kusini. Vile vile, kwa Tanzania Aflife daima imekuwa
ikisifika kwa kuwa na huduma bora kwa wateja na kupewa alama za AA-na
kampuni ya viwango ulimwenguni ya Global Credit Rating (GCR) kwa nguvu
ya kifedha na ulipaji bora wa madai.”mabadiliko kutoka Aflife kuwa
Sanlam Life Insurance yatachangia utendaji wa kibiashara kwa kampuni.
"Kuna mipango ya kupanua soko la rejareja na kutoa huduma za ziada
zilizo endelevu katika ukuzaji wa biashara, wateja wa Sanlam Life
Insurance watapata bidhaa mpya zilizoboreshwa zaidi.”
Kupitia
Sanlam, wateja wetu watakuwa na amani ya kufanya biashara na kampuni
yenye masoko mengi Afrika inayoongoza katika kuimarisha ukwasi na
usalama wa fedha. Tunatazamia kutumia fursa hii kuimarisha biashara yetu
pamoja na uhusiano na wateja, washirika wetu, na zaidi mfumo wa Sanlam
wa kufanya biashara kwa wingi na wateja. Tunapenda kuwahakikishia wateja
wetu kuwa Sanlam ina historia ya miaka 97 ya utendaji kazi na
mahusiano bora na wateja wake.
Bw.
Kirk anaendelea kwa kusema, "Sanlam inajulikana kwa kauli mbiu ya
“Wealthsmiths™” ambayo ni kielelezo tosha cha kile tunachokifanya na
kuamini.Hiii na wakilisha itikadi ya uhalisia wa namna ya utendaji kazi,
falsafa na uthamini wa rasilimali tunayoifanyia kazi ambayo ni fedha ya
wateja wetu.Tunaelewa kiundani kuwa ukwasi unahitaji utendaji wa hali
ya juu n akujitoa, kwa kutambua hili tunashirki kikamilifu na kwa
umakini.” Huduma zetu zinauhalisia wa kile ambacho tunacho kithamini na
pia tunafuata mfumo wa Sanlam ambao ni ujasiri, imani pamoja na ushujaa.
Kwa kufuata mfumo na utamaduni huo, huduma zetu zimekuwa bora zaidi
siku zote.
Ikiwa
na rekodi ya zaidimiaka 97, umoja wa makampuni ya Sanlam ina huduma
tofauti za kifedha pamoja na mali zisizohamishika zenye thamani zaidi ya
dola za Kimarekani bilioni 60na imesambaa sehemu mbalimbali duniani.
SEM(Idara Ya Masoko yanayokuwa)inawajibika kwa huduma za kifedha za
Sanlam kwa biashara katika masoko yanayokuwa nje ya Afrika Kusini, na
inalenga kuhakikisha utoaji endelevu wa huduma na ukuaji katika biashara
mbalimbali kwa kutumia nguzo hii
Picha ya Pamoja Mara Baad ya UzinduzI huo
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda Akitoa Hotuba yake
ambapo alipongeza Kampuni hiyo kwa Kuwa Mfano wa Kuigwa na Kuitaka
Kuongeza Juhudi zaidi ili kupiha hatua.
No comments:
Post a Comment