Na Avila Kakingo.
VIJANA waliotimiza miaka 18 kwa mwaka huu waaswa
kupiga kura ili kumchagua kiongozi wanaemtaka na watambue mchango wao katika jamii
kwa kupiga kura kwaajili ya maendeleo ya
taifa letu.
Nae Mwenyekiti wa
asasi isiyo ya kiserikali Tanzania People with Disabilities Organization (TAPWAO),
Michael Mwanzalima ameomba tume ya
uchaguzi kutoa vipaumbele kwa walemavu wa viungo mbalimbali siku ya kupiga
kura ili isiwe kikwazo kwao katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili
waweze kuwachagua viongozi wanao wafaa.
Hayo yamesemwa na vijana mbalimbali waliohudhuria katika mdahalo
wa “ELEKEA UCHAGUZI 2015 NA VIJANA ”ulioandaliwa na kampuni ya Tanzania Bora Initiative (TBI) ikiwa
na nia ya kuadhimisha siku ya vijana dunia katika mdahalo uliofanyika katika
hoteli ya New Afrika Dar es Salaam leo.
Pia katika mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali hapa
nchini ikiwa na wacheza muvi,waimba mziki wa kizazi kipya (Bongo freva) na
vijana kutoka makampuni mbalimbali wakijadiliana kuhusiana na UCHAGUZI MKUU WA
OKTOBA 25 MWAKA HUU, vijana watashiriki vipi ili kuchagua kiongozi wanae mtaka.
Pia katika mdahalo huo uliambatana na uzinduzi rasmi wa kampeni ya njia ya mtandao
ya habari ujulikanao kama UCHAGUZI 2015#
KURA YETU.
Mbunge
wa viti maalumu (CCM) Maria Salungi akichangia maada kuhusiana na
kijana anajitambuaje katika kuhamasika kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu
ili waweze kumchagua kiongozi wanae mtaka, kwa kuwa baadhi ya vijana ni
mara yao ya kwanza upiga kura.
Le
Mutus akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Tanzania Bora
Initiative uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam
jana.
Mwigizaji
wa Bongo Muvi Rose Ndauka akichangia maada kuhusiana na waandishi wa
habari vijana wanaweza kusaidia zaidi katika kufikisha ujumbe kwa vijana
wengine ili waweze kwenda kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
utakao fanyika Oktoba 25 aliyazungumza hayo katika mdahalo uliofanyika
katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana.
Mwenyekiti wa
asasi isiyo ya kiserikali hapa nchini ya Tanzania People with Disabilities Organization (TAPWAO),
Michael Mwanzalima akizungumza katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana, yeye akiwakilisha walemavu akiomba rai kwa Tume ya uchaguzi kuwawekea mazingira rafiki katikauchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 waweze kupiga kura bila kikwazo chochote.
Baadhi ya vijana waliohudhulia katika mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
wageni waalikwa wakiwa katika mdahalouliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
Manzilishi
wa kampuni ya Ekihya na mwenyekiti wa mdaholo uliofanyika katika hoteli
ya New Afika jijini Dar es Salaam.akizungumza na vijana waliohudhulia
mdahalo huo.
Humphrey Pole pole akizungumza katika mdahalo uliofanyika
katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam. akiwaasa vijana
wajitokeze katika upigaji kura wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 25 ili
kuwachagua viongozi bora na sio bora viongozi.
Bandi
ya muziki ambayo jina lake halikuweza kupatikana ikitumuiza katika
mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo.
No comments:
Post a Comment