Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika
ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti Visiwani na Rais
wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa
kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya
CCM mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani na
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu
Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania
urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya
kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao
Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Bernard Membe na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose
Migiro wakipongezana baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya
wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla
ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (kushoto) akimpongeza Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama,
Bernard Membe baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania
urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya
kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao
Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu
Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania
urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya
kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao
Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) (NEC) wakimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), baada ya
kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu
ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC,
katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
No comments:
Post a Comment