Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli
wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Juni 18, 2015. Picha zote na CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Balozi
wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki
wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika
katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Dk. Patrick Bergin
akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya sifa ya wanyamapori
katika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza na
waandishi wa habari leo katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Juni 18, 2015.
Balozi
wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii Jacqueline
Mengi kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli
wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Juni 18, 2015.
Balozi
wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki
wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari.
Viongozi wa Dini waliofika katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa kampeni hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa pamoja na Viongozi wa dini na mabalozi wa kampeni hiyo.
---
Lengo
la WildAid ni kukomesha biashara haramu ya wanyama pori kwa kupunguza
mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori kupitia kampeni za
uhamasishaji.
Pia
lengo la WildAid ni kutoa hifadhi na ulinzi wa uhakika kwa viumbe wa
baharini. Biashara haramu ya wanyama pori inakadiriwa kuwa na thamani ya
zaidi ya dola bilioni 10 kila mwaka na imesababisha kupungua sana kwa
wanyama pori sehemu mbalimbali duniani.
Kama
ilivyo biashara ya madawa ya kulevya, uwepo wa sheria dhidi ya biashara
hiyo na jitihada za kuhakikisha utekelezaji wa sheria havijaweza kuleta
ufumbuzi wa tatizo hili. Kila mwaka, mamia ya mamilioni ya dola hutumika
kuwalinda wanyamapori, lakini kiasi kidogo kukomesha mahitaji ya viungo
vya wanyama pori na bidhaa zitokanazo na wanyama pori.
WildAid
ndio shirika pekee ambalo limelenga kupunguza mahitaji kupitia ujumbe
rahisi usemao: UNUNUZI UKIISHA, MAUAJI NAYO YATAISHA.
WildAid inafanya kazi na mamia ya watu mashuhuri katika bara la Asia na nchi za Magharibi hususani wanasiasa mashuhuri, watu maarufu na viongozi wa makampuni makubwa wakiwemo Mrithi wa Ufalme wa Uingereza Prince William, Yao Ming, Jackie Chan, Li Bingbing na Sir Richard Branson ili kuwashawishi watu waache kununua bidhaa zitokanazo na wanyama walioko katika hatari ya kutoweka. Hivi sasa ujumbe huu na jitihada kuelimisha watu zinawafikia mamia ya mamilioni ya watu nchini China kila wiki kupitia matangazo mbalimbali.

No comments:
Post a Comment