Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Zena Kongoi.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Zena
Kongoi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
mchana, kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea
katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na shirika
hilo katika miradi mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali
Watu na Utawala wa Stamico, Deusdedith Magala.
Madini mbali mbali yaliyopo katika banda la shirika hilo.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Madini la Taifa (STAMICO) limeanzisha miradi mbalimbali ya
kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini ili kuwaendeleza kutoka katika
uchimbaji duni usiozingatia kanuni.
Kuanzishwa
kwa miradi hiyo kunatokana na wachimbaji hao kutokuwa na maeneo maalum
ambapo itawasaidia wachimbaji hao kufikia kiwango cha uchimbaji wa kati
chenye tija, ambapo ni muendelezo wa mradi wa kuratibu na kuwaendeleza.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo maonesho
ya wiki ya utumishi wa umma yanafanyika jijini Dar es Salaam leo mchana,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Zena Kongoi alisema shirika
hilo limepata mafanikio mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2014 hadi
mwaka huu wa 2015.
Alisema
kupitia mradi huo, shirika limeweza kuwawezesha wachimbaji wadogo wa
madini ya bati wa Wilaya ya Kyerwa kupata soko la madini hayo, jambo
ambalo limesaidia kupunguza utoroshaji wake kwenda nchi jirani na
kuiongezea serikali mapato.
"Tumewawezesha
kwa kuwapa ushauri wa kitaalamu na kiufundi kwa wachimbaji wadogo
mbalimbali. Lakini pia tunaelekea kukamilisha mchakato wa mfumo mtandao
wa uchimbaji mdogo utakaowawezesha kupata taarifa sahihi na kwa wakati
kuhusu masoko, bei n aina bora za vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji,"
alisema.
Kongowi
alisema kwenye mradi wa dhahabu unaosimamiwa na kampuni tanzu ya
Stamigold Biharamulo Gold Mine, mgodi huo umeweza kuingiza Dola za
Marekani milioni 14.2 katika kipindi cha Agosti, mwaka jana na Mei,
mwaka huu.
Aliongeza
kuwa mgodi huo pia umeanza kulipia ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 kwa
halmashauri ya Biharamulo na kuchangia pato la taifa kwa kurejesha
mrahaba wa asilimia 4, ambapo wanatarajia kupata Sh. milioni 609 kama
ada ya usimamizi wa mgodi huo.
Mbali
na mafanikio hayo alisema zipo baadhi ya changamoto ambazo wanaendelea
kuzishughulikia ambapo miongoni mwake ni upungufu wa mtaji kutokana na
kuwa shirika hilo kwa sasa linafufua upya miradi yake mingi.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu, Deusdedith Magala
alisema, kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu ya maonesho hayo, shirika
hilo linahakikisha linawasaidia akinamama kwa kuwatengezea mazingira
mazuri ya kufanya kazi ndani ya shirika hilo.
Aliongeza
kutokana na shirika hilo kuanza kazi upya katika kipindi cha mwaka jana
walilazimika kuajiri wafanyakazi wapya 87 ambapo wanawake ni 25 na
wanaume 62 lengo likiwa ni kuwezesha shirika hilo kusonga mbele. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com simu namba-0712-727062)
No comments:
Post a Comment