Teknolojia na Maisha : TIGO Yatoa dola laki moja na nusu kwa hospitali ya CCBRT Kusaidia watoto wenye miguu iliyopinda - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 19 June 2015

Teknolojia na Maisha : TIGO Yatoa dola laki moja na nusu kwa hospitali ya CCBRT Kusaidia watoto wenye miguu iliyopinda


 Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kusisaidia Hospitali hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans na Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans akizungumza katika hafla hiyo.
 Meneja  Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT baada ya kutiliana saini mkataba wa kusaidi matibabu ya ulemavu wa miguu Dar es Salaam jana. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute na Meneja Uwajibikaji kwa Jamii, Woinde Shisael.
 Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Picha mbalimbali zikionesha miguu iliyopinda.
 Wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Joyce Moshi akiwa amembeba mtoto wake Gedion ambaye anatibiwa katika Hospitali hiyo kutokana na miguu yake kupinda ambapo sasa anaendelea vizuri.

Na Dotto Mwaibale
HOSPITALI ya CCBRT, imepokea dola 150,000 (zaidi ya sh. mil. 320) kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa ajili ya kugharamia matibabu ya watototo wanaozaliwa na ulemavu wa nyayo zilizopinda kwa miaka mitatu ijayo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema hiyo si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kugharamia matibabu ya walewavu kwani miaka mitatu iliyopita pia waligharamia matibabu ya watoto wenye ulemavu wa midomo.

"Tuna amini watoto wenye ulemavu wa unyayo uliopinda watapatiwa matibabu mapema, hivyo tunaomba wazazi wenye watoto wao wanaozaliwa na ulemavu huo kujitokeza CCBRT kupatiwa matibabu kwani ni bure na kwa mwaka tunatoa dola 500," alisema Gutierrez.

Kwa upande wa Daktari wa Mifupa wa hospitali hiyo, Prosper Alute akizungumzia ugonjwa huo, alisema unasababishwa na kurithi kutoka kwa wazazi au ndugu na kunywa pombe kupindukia au kutumia dawa zenye viambata kali.

Alisema asilimia 50 ya watoto wanaozaliwa hupata ugonjwa huo kwa miguu yote ambapo tangu kuingia kwa mwaka huu hadi Aprili, watoto 117 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo ambao ni sawa na wastani wa watoto 10 kwa wiki.

Alisema ugonjwa huo usipotibiwa kwa haraka unaweza kumsababishia mtoto kutembea kwa shida na wakati mwingine kutotembea kabisa.

Kwa upande wa Joyce Mosha, Mkazi wa Mwenge,  ni mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake, Gidion ana miezi miwili alikutwa na tatizo hilo na kufanyiwa upasuaji, alisema mara baada ya kujifungua madaktari waligundua mtoto wake kuwa na tatizo hilo, hivyo waliamua aanze kupatiwa matibabu.

"Namshukuru Mungu alifanyiwa upasuaji mdogo na hivi sasa anaendelea vizuri, alipogunduliwa ana tatizo hilo kwanza walimfunga plasta ngumu (POP) kwa wiki tano na kisha kumfanyia upasuaji mdogo wa mfupa na kumpa viatu maalumu vya kuvaa na vingine huwa anavaa usiku tu wakati wa kulala," alitoa ushuhuda Joyce. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712727062)

No comments:

Post a Comment