Matukio : Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa - Yatoa Mafunzo ya Menejimenti ya Maafa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 6 June 2015

Matukio : Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa - Yatoa Mafunzo ya Menejimenti ya Maafa

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Florens Turuka (wa kwanza kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi alipokuwa akiwasili katika Viwanja wa Baraza la Maaskofu Kusarani wakati wa mafunzo kuhusu Menejimenti ya Maafa kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo, Juni 4, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya akieleza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya kuhusu Menejimenti ya Maafa katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam, Juni 4, 2015.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifanya zoezi la kuzima moto baada ya mafunzo ya kujiandaa na kukabiliana na dharura ya moto Juni 4, 2015 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Mwezeshaji wa mada ya Menejimenti ya Maafa Bi. Naima Mrisho (hayupo pichani) wakati wa mafunzo yaliyoratibiwa na Idara Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini, Dar ea Salaam Juni 4, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Florens Turuka (wa kwanza kulia) akiteta jambo viongozi wa Ofisi hiyo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenza wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamiliwatu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi na katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya mara baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam Juni 4, 2015.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiiza Mkufunzi wa masuala ya kujikinga na dharura ya moto kutoka Chuo cha Zima moto Bw. Rajabu Mwangalamo wakati wa Mafunzo ya Menejimenti ya Maafa yaliyofanyika Baraza la Maaskofu Kurasini Dar es Salaam Juni 4, 2015.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifanya zoezi la kuzima moto baada ya mafunzo ya kujiandaa na kukabiliana na dharura ya moto Juni 4, 2015 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment