Mkuu
wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma,
Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma
taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu)
aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi
ya mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na
Kongo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Mkurugenzi
wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Harrison Mseke (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa
kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (wa nne kulia) akitoa
maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa
tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa taarifa kwenye kambi
ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi
ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu
wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick
Nisajile akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe wakati akitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi
ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole wakikagua sehemu wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea
kuwasili katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi wa Waomba hifadhi hao wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.
Muonekano
wa moja ya chumba cha kulala familia za waomba hifadhi katika kambi ya
Nyarugusu ambapo kifika muda wa kulala wanatandika mkeka chini katika
vumbi hilo jekundu na kupata usingizi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu),
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole (kushoto) wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa
Waomba hifadhi wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu
iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma walipotembelea kambi hiyo kukagua
kambi hiyo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna
ya kuzitatua.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu)
akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati
walipotembelea kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa juma lililopita.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akigawa vifaa vya
matumizi ya nyumbani ambavyo ni Blangeti, Mkeka, Kontena la kuhifadhi
chakula na dumu la maji la lita 10 kwa mmoja wa Waomba hifadhi
waliowasili siku ya ziara ya kutembelea kambi ya Nyarugusu mwishoni mwa
juma wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (mwenye shati jeupe).Kulia ni Mkuu wa
kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Waomba hifadhi na familia zoa wakiwa katika foleni ya kupokea vifaa hivyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na Waomba
hifadhi katika kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kutembelea
eneo hilo akiwa ameambatana na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
pamoja na Mwakilishi wa shirika la kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR).
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN)
Tanzania, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wakinamama anayeishi kwenye
kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakati wa ziara maalum ya kutembelea
maeneo hayo iliyohusisha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu
wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa
Ia Uhamiaji (I.O.M) (katikati) ambaye jina lake halikuweza kupatikana
kiurahisi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Harrison Mseke (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Mh. Mathias
Chikawe alipotembela katika chumba maalum kichotumika kufanya usajili
kwa Waomba hifadhi na familia zao kwa ajili ya kupewa hati ya kuwa
Wakimbizi kamili kama watatimiza vigezo vinavyohitajika. Aliyeketi kulia
ni Msajili wa Waomba hifadhi, Ndalo Charles Bogohe.
Zoezi la usajili likiendelea kwa familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wakinamama wakiandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama walivyokutwa na kamera ya modewjiblog.
Sehemu
ya familia za Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu,
wilayani Kasulu, mkoani Geita wakiendelea kujipanga baada ya kuwasili
kwenye eneo hilo.
Moja
ya familia za waomba hifadhi ikiwa imejipumzisha mara baada ya chakula
cha mchana huku nyuso zao zikionekana kuwa na furaha na matumaini mapya.
Hili ni eneo ambalo Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wa kambi ya Nyarugusu wakiteka maji safi kwa matumizi yao.
Mkurugenzi
wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Harrison Mseke (kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati wakielekea kukagua vyumba vya
madarasa katika shule ya msingi Mapendo ambayo yamegeuzwa kuwa nyumba za
kulala Waomba hifadhi, kutokana na uhaba wa makazi ya kuishi kwenye
maeneo ya kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine
pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma katika msafara huo.
Baadhi
ya Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakiwa
wamempumzika huku wengine wakipata chakula cha mchana kama walivyokutwa
na kamera ya modewjiblog.
Kinababa nao hushiriki kuandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama huyu aliyekutwa na kamera ya modewjiblog.
Eneo
la shule ya msingi Mapendo katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu ambalo
kwa sasa linatumika kuhifadhi Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili
nchini wakitokea Burundi kupitia mji wa Kigoma.
Madawati
ya wanafunzi katika shule ya msingi Mapendo yakiwa nje ya madarasa
yakitumika kuanikiwa nguo na huku wakati wa msimu wa mvua yakinyeshewa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakibadilishana mawazo na wasimizi wa kambi
hizo za Nyarugusu wakati wa ziara ya siku moja wilayani Kasulu, mkoani
Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa ameambatana na Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakikagua eneo jipya
litakaloitwa Nyarugusu B lililotolewa na serikali kwa ajili ya Waomba
hifadhi wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma ambalo liko mbioni
kutengenezwa na kukamilika ndani ya miezi 3 ijayo.
Eneo
jipya la kambi ya Nyarugusu B ambalo limetengwa na serikali ya Jamhuri
ya Tanzania kwa ajili ya makazi ya Waomba hifadhi wanataotenganishwa
Burundi na Congo mara tu baada ya kukamilika.
Muonekano
wa eneo jingine la makazi ya Waombahifadhi ndani ya kambi ya Wakimbizi
Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Amani
na upendo itawale kati yetu......ndivyo wanavyosema kwa pamoja baadhi
ya watoto waomba hifadhi wakifurahia picha pamoja na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez.
Na Modewjiblog team, Kigoma
WAKATI
dunia kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahangika kutanzua
changamoto za wakimbizi Nyarugusu, mkoani Kigoma imeelezwa kuwa idadi
kubwa ya Wakimbizi waliorejeshwa nchini Burundi kutoka kambi ya Mtabila
iliyoko Kigoma iliyofungwa rasmi Desemba, 2012 wameingia tena nchini na
kujazana katika makazi ya muda ya Nyarugusu wakiomba hifadhi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Sospter Christopher wakati
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekwenda kuangalia
hali halisi ya kambi ya Nyarugusu na Wakimbizi akiambatana na Maofisa wa
Umoja wa Mataifa akiwemo Mratibu wa Mashirika hayo nchini Alvaro
Rodriguez. Kurejea kwa wingi kwa Wakimbizi hao ni pigo kisaikolojia kwa
watu ambao walirejeshwa nyumbani kwa kuonekana kwamba hali ni shwari na
walikuwa wameanza kuishi maisha ya kawaida.
Mkuu
huyo wa kambi alisema idadi hiyo ikichanganyika na wengine imafanya
kambi kuhemewa na kuonekana haja ya kutafuta eneo jingine la kupiga
kambi kwa ajili ya Wakimbizi hao ambao mpaka mwishoni mwa wiki iliyopita
walikuwa zaidi ya elfu 51.
“
Kwa sababu tunapokea idadi kubwa ya waomba hifadhi toka Burundi,
tumekuwa tukiongeza idadi ya vituo vya mapokezi ili kukidhi mahitaji ya
kuwapokea wakati tukisubiri maelekezo toka ngazi za juu za kuwahamishia
Migunga Hills eneo linalopendekezwa kufunguliwa kambi ya Nyarugusu B”
alisema Christopher mbele ya Waziri Chikawe.
Alisema
walianza kupokea waomba hifadhi hapo kambini kuanzia Aprili 29, 2015
kwa idadi ndogo kabisa ya watu 36, lakini idadi hiyo ilianza kuongezeka
siku hadi siku na kufikia Mei 27 mwaka huu idadi yao ilifikia 48,333,
idadi kubwa ikiwa wanawake na watoto. Wakimbizi hao walikuwa wakipitia
vituo vya Kigoma (27,638), Manyovu (4,439), Kilelema (1,603) na Kigadye
(1,291).
Kambi
hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 50,000 imeelemewa kwa sababu ya ujio
mpya uliosababisha kuwepo kwa Wakimbizi zaidi ya 106,410.
Kuna
matatizo zaidi ya milipuko ya wagonjwa kambi hii imechanganywa na
Wakimbizi wa Kongo watu ambao hawana utamaduni wa pamoja na kuonekana
hatari ya kukabiliana kwa kutosikilizana. Aidha kambi hiyo pamoja na
kuwahifadhi waburundi wapo pia Wakimbizi kutoka Kongo wapatao 54,706;
Burundi,3261 ; Rwanda 72; Uganda 17; Sudan Kusini wanane; Kenya 7;
Somalia 3; Ethiopia 1; Zimbabwe 1; na Ivory coast 1.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari walioambatana naye katika ziara hiyo
kuhusu hali ya baadae ya Wakimbizi wa Kongo ambao wapo nchini kwa
takribani miaka 19 sasa, Waziri Chikawe alisema kwamba serikali haina
mpango wa kuwapa uraia kwa sasa ingawa Marekani imesema itawachukua
Wakimbizi elfu 30 kuwapeleka kwao na kwingine duniani.
“hatuna
mpango wa kuwapa uraia kwa sasa…” alisema Chikawe na kusema kwamba kwa
kuondolewa kwa hao wengine kutasaidia kupunguza idadi yao katika kambi
hiyo. Alisema kwamba ni lengo la serikali kuhakikisha kwamba kambi hiyo
inapunguzwa ili kuweza kuchangia ipasavyo kwa hali bora ya Wakimbizi na
kwamba mchakato wa kuwaangalia waomba hifadhi kama wanafaa kuwa
Wakimbizi unaendelea.
Akizungumzia
malalamiko ya upatikanaji wa chakula, Waziri Chikawe alisema kwamba si
kweli kuwa kuna watu hawajapata chakula kwa siku saba la sivyo
wangelikufa. Alisema wengi wa Wakimbizi ni watoto na kwamba wanapoingia
nchini wanapewa vyakula vikavu (kama biskuti) lakini wakishafika kambini
wanapewa chakula kilichopikwa na resheni ya siku 14 .
Alisisitiza
kuwa kama kungelikuwa hakuna chakula watoto hao wasingeishi, labda kama
wanataka kuongezewa chakula zaidi. Kuhusu ujenzi wa kambi mpya Migunga
alisema kwamba wataalamu wanaangalia barabara mbadala kwani iliyopo sasa
pamoja na kuhitajika milioni 300 kuitengeneza lakini bado kila mvua
itakapokuwa inanyesha itahitaji kutengenezwa.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole katika mahojiano na waandishi wa habari
aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kufungua mipaka ili Wakimbizi
waweze kuingia na kutoa eneo kwa ajili ya kambi mpya kutokana na ya sasa
kujaa sana.
Aidha
aliishukuru serikali ya Uingereza kwa kuwa ya kwanza kutoa misaada kwa
ajili ya Wakimbizi hao na kutarajia nchi nyingine kama Marekani itafanya
hivyo mapema ili kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuhudumia waomba
hifadhi. Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro
Rodriguez amesema wanafanya kila linalowezekana ili kupunguza idadi ya
Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu kwa kuwapatia eneo jingine la
kujihifadhi.
Alisema
kwa kuwatoa hapo watasaidia shule zilizofungwa ambazo zinasomesha
watoto kutoka kwa Wakimbizi wa Kongo kurejea madarasani kukamilisha
mtaala wao.
No comments:
Post a Comment