Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa
Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika
Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa
Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama
hizo kutoka mataifa Mengine.Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri
Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania
poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya
mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya
kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora
vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini
zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata
fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za
LuvTouch Manjano ukumbini.
Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza
Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa
Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari
alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa
Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa
Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .
Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation,
ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo
zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato
na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha
yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake,
Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha
wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.
Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania
kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na
kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha
Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua
pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa
kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser
Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda
(Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi
ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv
Touch.
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani
ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya
Luv Touch
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bongo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa
Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda
wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi
Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa
Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka
Uganda.
wageni walikwa
No comments:
Post a Comment