HISTORIA FUPI YA BIASHARA YAKO;
Sina muda mrefu toka nimeanza hii biashara.Ilianza rasmi mwaka jana mwishoni.
Kilichoniinspire ni baada ya kupata ujauzito nilihangaika sana kupata mafuta ya nazi kwa ajili ya mtoto.Kile kipindi cha maandalizi nilitafuta sana mafuta ya nazi sikupata.Kila ukiwauliza waliokutangulia katika malezi kuhusu mafuta ya kumpaka mtoto mchanga wanakwambia ya nazi.Nikitafuta madukani hamna hasa maduka ya watoto ila nikakumbuka mie najua kutengeneza mafuta ya nazi.Hivyo nikatengeneza mafuta mwenyewe nikayahifadhi kwenye bag langu la clinic tayari kusubiri siku ya kujifungua.
Nilipopata mtoto nikawa namtengenezea mwenyewe nyumbani.Wazo likaanza kuniingia kwa nini nisitengeneze mafuta maalum ya nazi kwa ajili ya watoto?Ndio mafuta ya nazi hata mtu mzima anaweza kupaka ila ni uamuzi wake lakini kwa mtoto nazi ndio mafuta muafaka.
Basi mwanangu alipofikisha miezi 6 nikaanza mchakato.Kufatilia masoko ya nazi,chupa za kuwekea branding kwa ujumla,changamoto zilizopo za biashara husika,nikajitosa.Nikatoa chupa 100 za majaribio zikanunuliwa zoote kwa muda mfupi ndio nikaona nianze sasa.
Nikaanza kutoa na kuweka maduka matatu duka la mwanzo lilikuwa glamarous la wanawake lipo sinza,la pili funzone la watoto lipo mbezi beach shamo tower na la tatu zero 2 twelve lipo Namanga.Kidogo kidogo nikaanza kusambaa na maeneo mengine.
Mafuta haya kwa sababu nimelenga watoto yanapatikana zaidi kwenye maduka yanayouza nguo na vifaa mbalimbali vya watoto,saloon za watoto.Pia kwenye boutique na saloon za akina mama.
Chupa ya mls 200 inauzwa tsh 10,000.
MATARAJIO YAKO YA BAADAE;Matarajio ni biashara yangu isambae Tanzania nzima.Na niwe nimeleta suluhisho la wakina mama kuhangaika kutafuta mafuta ya nazi kwa ajili ya watoto wao.
1.Zurii house of beauty duka lipo Dar free Market shop no F4,
2.Naikite Pharmacy Mwenge,Tabata Magengeni katika saloon ya watoto inaitwa Lb Kids barabarani karibu na crdb bank simu 0652643614,
3.Duka la watoto la zero twelve namanga inatazamana na mMog restaurant ambayo zamani iliitwa nyumbani lounge 0716454580,
4.Duka la vifaa vya watoto linaitwa funzone lipo mbezi beach samaki jengo la shamo tower,
5.Duka la nguo za wadada na wanawake the glamarous fashion lipo sinza mapambano,
6.Ilala mtaa wa Arusha kwenye min supermarket ya Alu Mart ,
7.Kariakoo yapo duka la watoto Kids fashion lipo mtaa wa Mkunguni karibu na stand ya mabasi ya tegeta 0715234588,
8.Kimara unashuka kimara stand then unaelekea njia ya morogoro road ya zamani kwenye kona inayounganisha barabara ya golani na morogoro road ta zamani utaona duka la love baby classic wear lipo kushoto kama unaelekea golani simu 0719382095.
Temeke yapo boutique ya akina mama DEENS STORE lipo kituoni kabisa kwa azizi ali yanaposimama mabasi ya kwenda mbagala.
Tegeta yanapatikana SUMSKAYA MOTHER AND CHILD SHOP tegeta nyuki/kibaoni
ARUSHA
Yapo sakina TWINS COSMETICS SHOP pembeni ya sakina bar
DODOMA
Yapo OSF STATIONARY oposite na sido na johari design karibu na msikiti wa majengo.Maeneo ya uhindini.jamatini,sabasaba kotee.
No comments:
Post a Comment