Meneja
wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji
nchini (EPZA), Mhandisi Keneth Haule (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi
ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri.
Wengine pichani ni Bw. Abel Shirima (Kushoto), Bw. Aloyce Andrea (Wapili
Kushoto), na Bw. Omary Abdallah (Wapili Kulia).
Kiongozi
wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo
(Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya
kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka,
Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Mkurugenzi
wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) akizungumza na Kiongozi
wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) wakati Bibi Mwanri na ugeni wake walipotembelea Ofisi za
Mamlaka kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika
Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa
Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Bibi
Lilian Kalengo (Kulia), muwakilishi wa Kiwanda cha Tooku Garments
akiwaonesha suruali ya jeans wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati
inayotekelezwa eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini
(EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda 12
vilivyoanza uzalishaji katika Ukanda wa huo.
Kiongozi
wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) akiangalia moja ya suruali zinazotengezwa na kiwanda cha Tooku
Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa
Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa mabinti wa Kitanzania walioajiriwa na Tooku Garments akiwa kazini.
Wakina
dada wakiendelea na kazi ya utengenezaji wa suruali za jeans
zinazotengenezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la
Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar
es Salaam.
Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI
No comments:
Post a Comment