Kijana Daudi Mrindoko aka Obama wa Moshi ana umri wa miaka 30
Daudi Mrindoko akiwa na Mama Minde Mwenyekiti wa CCM Moshi mjini
Buberwa Jackob, Moshi,Kilimanjaro
Wakati
tunahesabu miezi kuelekea uchaguzi mkuu 2015,mengi ya kufurahisha
yanahibuka kama vile wananchi wa jimbo la Moshi Mjini kumshawishi
mgombea waokijana Daudi Babu Mrindoko achukue fomu ya kugombea ubunge wa
jimbo hilo 2015,na kumiminia sifa zote zinazofaa kijana huyo wa mjini
Moshi achaguliwe.wakazi hao wa jimbo la Moshi Mjini kwa sasa wanadai
kuwa kijana wao waliomshawishi achukue fomu ndiye Mgombea kijana mwenye
umri mdogo kuliko wengine wote wenye nia ya kugombea ubunge mkoani
Kilimanjaro,kwani Daudi Mrindoko ana umri wa miaka 30 tu, na hakuna wa
mgombea yoyote hadi sasa mwenye umri chini ya miaka 30 mkoani
Kilimanjaro. Wenyewe wakazi wa jimbo la Moshi mjini wanadai kuwa kijana
huyo mdogo ndio pendekezo na tumaini lao la uchaguzi 2015,na wanahidi
kumpa kila wawezalo bila kujali atagombea kwa kupitia tiketi ya chama
gani,wanachojali uwezo wake wa kuwatumikia na kuwawakilisha bungeni.
Kijana
Daudi Babu Mrindoko(30) ni mkazi wa Moshi mjini,Mjumbe wa UVCCM mkoa
Kilimanjaro,pia mwenyekiti wa tahasisi ya Umoja wa wazalendo
Tanzania(UWATA) inasemekena ni kijana mwenye mvuto sana kwa jamii
kutokana na ukaribu huo wananchi wa jimbo la Moshi mjini uwambii
chochote juu ya kijana wao huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye wamempa
majina mengi
kama a.k.a Obama wa Moshi, na kauli mbiu ya ni "Moshi Panafukuta Moto 2015' Pendekezo hilo la wana Moshi mjini pia linapatikana at www.facebook.com/mrindoko. mwidadi
No comments:
Post a Comment