Mkuu
wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akitoa
maelezo wakati wa kumpatia zawadi za kimila, Shuka ya rubega, mkuki na
ngao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia),
wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu
kwenye kampuni hiyo, na wengine 10 walizawadiwa kwa kufanya kazi kwa
kuzingatia sera mpya ya Acacia ya tabia sita (six desired behavior),
kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana
na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha
anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga
kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika
utendaji wa kazi wa kila siku. Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa wilaya
ambaye alikuwa mgeni rasmi, kwenye sherehe hiyo ambayo ilikuwa maalum
kuwatunuku wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya
Acacia, na kufanyika Alhamisi usiku wa kuamkia leo Ijumaa Mei 8, 2015,
aliwamwagia sifa wafanyakazi wa mgodi huo hususan uongozi mpya chini yaa
Brad, kwa kuja na sera mpya ambayo sio tu inawajali wafanyakazi bali
pia wananchi wanaozunguka mgodi huo ikiwemo serikali.
|
Brad
katika vazi la kiasili baada ya kutunzwa na wafanyakazi kwa kuleta
mabadiliko katika utendaji kazi wa migodi iliyo chini ya kampuni ya
Acacia, ikiwemo Buzwagi. |
|
Meneja
Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia udthabiti wa kampuni hiyo,
(GM-Organizational Effectiveness), Janet Reuben-Lekashingo, (kulia),
akimkabidhi cheti Isack John Nkulu, kwa utumishi wa muda mrefu kwenye
kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert
Rweyemamu. |
|
Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi, Blandina Munghezi,
(katikati), akipewa cheti cha utumishi wa muda mrefu katika kampuni ya
Acacia, inayomiliki mgodi huo. |
|
Brad, akimkabidhi tuzo ya ufanyakazi uliotukuka, Hashim Waziri, katukati ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu. |
|
Meneja
wa Biashara, (Commercial Manager), wankampuni ya Acacia, Jason Watson,
(kushoto), Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, (kulia), na
Meneja wa Mgodi wa North Mara anayeshughulikia uthabiti wa Mgodi,
(Effectiveness), Solomon Rwangabona, wakifurahia jambo. |
|
Michell, akiteta jambo na Rweyemamu, (kulia). |
|
Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hiyo. |
|
Michell akimpongeza Meneja anayeshughulikia uthabiti wa Mgodi wa Buzwagi, Sanga, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hiyo. |
|
Brad,
akimkabidhi cheti cha kutambua ufanyazi uliotukuka wa Thompson
Paraxceed Francis katika Mgodi wa Buzwagi huku Meneja Mkuu wa Mgodi
huoi, Filbert Rweyemamu akishuhudia. |
|
Wafanyakazi wakipatiwa utaratibu wakati wa kupokea zwadi na tuzo. |
|
Brad, akiwahutubia wafanyakzi wake. |
|
Meneja Mkuu, Rweyemamu akitoa hotuba yake. |
|
Simon Sanga, akitoa hotuba yake na kuelezea utaratibu na vigezo vilivyotumika kuwapata wafanyakazi bora na wale wa muda mrefu |
|
Mpesya,
Kushoto), a,kiagana na Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Mgodi wa Buzwagi,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mstaafu Jamal Rwambow, huku Meneja
Mkuu wake, Rweyemamu akishuhudia, mwishoni mwa hafla hiyo |
|
Wasanii
wa kikundi cha sanaa cha Kahama Medical Cultural GHroup, wakifanya vitu
vyao huku Tumbili (kushoto) nayw akiruka kufuata midundo ya ngoma |
No comments:
Post a Comment