Mbunge
wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni
mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Tundu Lissu akihutubia
umati mkubwa wa wakazi wa Jiji la Arusha katika viwanja vya Shule ya
Msingi Ngarenaro katika mkutano uliokuwa katika sura ya UKAWA kwa
kuwashirikisha NCCR Mageuzi.
Mkutano huo nusura uathiriwe na mvua
kubwa iliyonyesha wakati Mbunge wa Kigoma Kusini Mh David Kafulila
lakini mapenzi ya wafuasi wa CHADEMA kwa chama na viongozi wao
yaliwafanya wavumilie kunyeshewa mpaka mwisho. Viongozi walikataa
kukingwa na mvua hiyo na kujikuta wote wakilowa mwili mzima kama
wananchi wengine.
Katika hotuba yake, Mh Lissu aliwaeleza wakazi
wa Arusha kitendo cha Serikali ya CCM imeshakorofishana na karibu kila
kundi la jamii kwa kutaja wafanyabiashara, walimu, madaktari, madereva,
wafanyakazi n.k ni ishara kuwa chama hicho kimechokwa na kinaweza
kuondoka madarakani katika Uchaguzi wa mwaka huu ambao alisisitiza ni
lazima ufanyike.
Msafara
wa Viongozi wa UKAWA. Kutoka Kushoto Mbunge wa Arusha Mjini Godbless
Lema, Mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu, Mbunge wa Kigoma
Kusini Mh David Kafulila, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi
na mwanausalama wa CHADEMA
Mbunge
wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), Mh David Kafulila ambaye kwa siku za
karibuni amejizolea sifa lukuki kwa kuweza kuanzisha sakata la ESCROW na
kulisimamia mpaka mwisho bila kuhofia vitisho mbalimbali. Katika
mkutano huo Kafulila aliwashukuru wakazi wa Arusha kwa mapokezi mazuri
na kusisitiza kuwa anajisikia furaha sana kuhutubia umati mkubwa Jijini
hapa ambapo ni mji wa kihistoria katika harakati nyingi za kisiasa
nchini. Kafulila aliwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba wawe na
imani kupitia UKAWA na kwa kura zao wataweza kuitoa CCM madarakani.
Mwenyekiti
wa Baraza la Vinaja CHADEMA Taifa Mh Patrobas Katambi akihutubia
mkutanoni hapo ambapo aliataka vijana kutokubali kuyumbishwa na
wanasiasa wanaojaribu kuupotosha umma kuhusu ushirikiano wa vyama
vinavyounda umoja wa UKAWA. Katambi alisisitiza zaidi kwa kutolea mfano
wa ziara waliyonayo kwa pamoja na Mbunge Kafulila kuzunguka mikoa ya
Kaskazini. Pia aliwataka vijana kuwatayari wakati wowote kupinga jaribio
lolote la Serikali kuongeza muda wa kufanyika Uchaguzi Mkuu tofauti na
mwaka huu.
Mh
Godbless Lema akizungumza na wananchi wake hii leo ambapo alitumia muda
mwingi kuwatoa hofu dhidi ya propaganda zilizoeneo Jijini hapa kwamba
hatagombea Arusha Mjini tena na kwamba Jimbo la Arusha Mjini litarudi
CCM. Lema aliwaambia wazipuuze propaganda hizo na kuziita ni za kipuuzi
kwasababu hakuna namna ambayo CCM inaweza tena kuwashawishi wananchi wa
Arusha kuichagua. Alisisitiza kuwa kwa muda mfupi aliowatumikia mbali na
vikwazo vingi ameweza kutimiza wajibu wake kama mbunge kwa kiwango
kikubwa huku akiorodhesha mambo mablimbali aliyotimiza kwa yeye binafsi
na mengine kupitia madiwani wake.
Kwa pamoja, Mh David Kafulila na Mh Tundu Lissu walimuombea Mbunge Lema ruhusa kwa wananchi wa Arusha ili mbunge wao aendelee kufanya kazi ya siasa maeneo mengine nchini kuharakisha kile alichokiita ukombozi wa mara ya pili, na kwamba wasijikisike vibaya ama kudhani mbunge hakai nao Jimboni.
Kwa pamoja, Mh David Kafulila na Mh Tundu Lissu walimuombea Mbunge Lema ruhusa kwa wananchi wa Arusha ili mbunge wao aendelee kufanya kazi ya siasa maeneo mengine nchini kuharakisha kile alichokiita ukombozi wa mara ya pili, na kwamba wasijikisike vibaya ama kudhani mbunge hakai nao Jimboni.
Waheshimiwa Kafulila na Lissu wakipokelewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Kalist Lazaro mwenye tisheti)
Viongozi wa CHADEMa na UKAWA wakiimba wimbo wa Taifa sambamba na wananchi (hawaonekani pichani) kabla ya kuanza hotuba zao
Kutoka
kushoto waliokaa Mh Godbless Lema, Mh Tundu Lissu, Mh David Kafulila,
Mwenyekiti CHADEMA Arusha Mh Kalist Lazaro na Mwenyekiti CHADEMA Wilaya
ya Arusha Mjini Derick Magoma
Mh Kafulila akiteta jambo na Mh Lissu huku Mh Lema naye akiteta jambo na Mwenyekiti wa Vijana Arusha Mjini Mh Innocent Kisanyage
Mama na mwanae akiendelea kufuailia mkutano huku akisaidiwa kukingwa mvua
Mwenyekiti
wa Vijana CHADEMA, Patrobas Katambi akisalimia wakazi wa Arusha
waliojitokeza mkutanoni hapo baada ya kutambulishwa na Mbunge wa Arusha
Mjini Mh Godbless Lema
Mh Kafulila akitamulishwa Jukwaani
Wananchi wakiuatilia mkutano huku mvua ikiendelea kunyesha
Mh Kafulila akisalimiana na Katibu wa CHADEMA Arusha Mjini Mh Lewis Kopwe. Wanaonekana walivyolowa chapa chapa
Wananchi wamelowa lakini hawaondoki mkutanoni
Mh Lissu akiwa amelowa mwili mzima na bado anaendelea kuhutubia huku mvua inayesha
Kutoka kushoto; Kalisti Lazaro, Patrobas Katambi, David Kafulila, Godbess Lema, Derck Magoma
Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA Arusha Mjini wakifurahia jambo
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu Taifa (CHADEMA) ambaye pia ni mtangaza nia ya Ubunge
Jimbo la Same Magharibi, Kamanda Chritopher Mbajo akiteta na Mwenyekiti
wa Vijana CHADEMA Taifa Bw Patrobas Patambi, mwenye kombati
Mtia
nia wa Jimbo la Mkalama Singida, Kamanda George Gunda (mwenye kombati
nyeusi) kwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia hotuba ya Mh Tundu
Lissu (haonekani pichani)
Mh
Lema akiwatambulishwa viongozi wa Kata ya Ngarenaro na kueleza namna
walivyoingilia kati hujuma ya kuchimbua uwanja huo mkutano usifanyike.
Yupo diwani Doita
Msafara
wa viongozi ukuindoka uwanjani hapo mara baada ya mkutano kumalizika.
Wananchi waliwazonga kiasi cha kusababisha kazi ya ziada kwa
wanausalama.
Eneo
la uwanja wa Ngarenaro ambalo linadaiwa kupitishwa greda na
wanaodhaniwa kuwa watu wa pinzani wa CHADEMA Jijini hapa kwa nia ya
kujaribu kuzuia mkutano huu wa leo usifanyike eneo hilo, jaribio ambalo
halikufua dafu kwani watu waliyapanda matuta hayo kama vile hakuna kitu
na mwishowe kusawazika kiasi.
Bossi Mzito wa Blog ya Arusha 255 Blog (Seria Jr T) Akiteta Jambo naMwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi
PICHA ZOTE NA SERIAJr NA MAKABAYO
No comments:
Post a Comment