Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina
Kombani, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ( kati kati) akisisitiza jambo.
Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe ( kushoto ) akiwa na mwezeshaji wa mafunzi, Patrick Ngwila.
Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani,
ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kuelekeza nguvu zao vijijini
kwenye idadi kubwa ya wananchi na wazalishaji wa mali wanaohitaji huduma zao badala ya kung’ang’ania mijini pekee.
Kombani
alitoa changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku nne yaliyoanza
Mei 25 hadi kufikia 28, 2015 mjini Morogoro ya kuwajengea uwezo na
ufahamu wafanyakazi wanaunda Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA)
kutoka katika mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PPF,NSSF,LAPF,GEPF,NHIF na
ZSSF.
Hata hivyo alisema, mifuko
hiyo imekuwa ikikimbilia kutafuta wanachama katika maeneo ya mijini na
kushindwa kubuni mbinu mbadala za kuwafikia wananchi wengi wanaoishi
vijijini.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo kuwa, dhana iliyojengeka kutoka kwa Mifuko hiyo
kuwa vijijini hakuna watu wenye vipato sasa imepitwa na wakati kwa kuwa
wananchi wanaishi vijijini ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara ndogo ndogo ambao wanaouwezo mkubwa wa kuchangia mifuko hiyo.
Waziri
Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki(CCM) alisema ,
kutokana na mifuko hiyo kujikita katika maeneo ya mjini imekuwa ikitoa
huduma hiyo kwa asilimia 4 na endapo itajitoa kuwafikia watu wa maeneo ya vijijini inaweza kutoka hapo ilipo na kufikia asilimia 10 na zaidi.
“ Wilaya ya Ulanga pekee kuwa kuna kundi kubwa la wakulima,wafugaji na waendesha bodaboda” alisema na kuongeza kusema.
“ Mfano mfuko wa bima ya afya wao wamejitoa kwenda kuhamasisha na wananchi wengi wameweza kujiunga na kuchangia huduma za matibabu na sasa mifuko mingine ya hifadhi ya jamii inafaa kufuata nyayo hizo za kubuni mbinu mpya za kwenda maeneo ya vijijini kupata wanachama wengi” alisema Waziri Kombani.
Awali , Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshack Bandawe, alisema malengo ya kuanzisha Jumuiya hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa lengo moja ili kuhakikisha sekta ya Hifadhi ya
jamii inaimarishwa ili kuingiza Watanzania katika mifuko hiyo ili waweze
kunufaika nayo katika maisha yao.
“
Tunayo mifuko saba ya Hifadhi ya Jamii na imewafikia watu asilimia 4.5
...lengo ni kutoka hapo angalao kufikia wastani wa asilimia 10 “ alisema
Bandawe.
Katibu
Mkuu huyo ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa alisema, kupitia
Jumuiya hiyo sasa wataanza kuwaelimisha wananchi wote walioko rasmi
katika soko ajira na wale wasio rasmi waweze kukingwa na mifuko ya
hifadhi ya jamii .
Kwa
upande wake Mwezeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika nchi za
Afrika Mashariki na Kati, Patrick Ngwila,alisema kwa sasa wanaangalia
namna ya kuiboresha mifuko hiyo kwa kupata uzoefu wa namna ya mifuko
hiyo inavyofanya kazi katika nchi hizo ambayo imekuwa ikisaidia wananchi
hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini.
Kwa mujibu wa Mwezeshaji huyo kuwa, kupitia
mafunzo hayo wanaangalia namna ya kupata wanachama ambao ni Watanzania
wanaoishi nje ya nchi kuweza kuchangia kwenye mifuko hiyo wakiwa huko
na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment