Meneja
wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu
Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati
inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa
Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea
(Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.
Meneja
wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu
Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati
inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na
wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kaimu
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto)
akizungumza na ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda
kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari
ya Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma
za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri (Wapili
Kushoto).
Kiongozi
wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika
Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati
walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu
wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni
P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa
ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea
maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es
Salaam.
Kiongozi
wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) akizungumza wakati walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi
ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Pichani meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI
No comments:
Post a Comment