Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonesha Rais Jakaya Mrisho
Kikwete maeno yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko huko Tegeta
wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, tarehe 14/5/2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maagizo kwa uongozi
wa wilaya ya Kinondoni kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozunguka makazi ya watu
eneo la Tegeta wilayani Kinondoni kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf
Mwenda akiwaagiza kutafuta mbinu za kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozingira
makazi ya watu eneo la Tegeta.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia makazi holela
yaliyojengwa katika bonde la mkwajuni eneo la mto Msimbazi na kisha kuongea na
wakazi wa eneo hilo akiwashauri kuhama kwakuwa eneo hilo si salama kwa maisha
na mali zao
No comments:
Post a Comment