Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu
wa Chama Cha Walimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya
Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo
wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama
Hicho.Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua
changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy
Maro)
Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na
walimu waliofika katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
unaoendelea jijini Arusha .Jumla ya walimu 1000 wanahudhuria mkutano
huo kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiteta jambo na
mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko
jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho jijini Arusha.Jumla
ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali
nchini.
Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiwasili katika
ukumbi wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea
jijini Arusha .Jumla ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka
sehemu mbalimbali nchini ambapo Raisi Kikwete alihutubia.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akizungumza jambo
na mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko
jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho. Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand
Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Raisi Jakaya Kikwete amesema kuwa walimu watarajie nyongeza
ya mishahara itakayoanza mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni moja kati ya jitihada
za serikali katika kuboresha maslahi ya walimu nchini.
Kikwete akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT ) uliofanyika jijini Arusha jana amesema kuwa nyongeza hiyo itahusisha
walimu wote wanaolipwa kima cha chini
cha mshahara na kima cha juu pasipo kutaja kiwango kilichoongezeka.
“Wakati mnachukua mishahara yenu benki mwezi Agosti mtaona
tofauti ambayo ni nyongeza ya msahara ,wenzenu wa chama cha Wafanyakazi
waliniomba nisitangaze niongeze kimya
kimya ili wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa” Alisema Raisi Kikwete
Aidha Raisi Kikwete alisema kuwa serikali inaendelea na
jitihada za kuhakikisha kuwa inaboresha elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha
maslahi ya walimu nchini,kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia,nyumba za
walimu,vitabu na maabara.
Amesema kuwa madai ya walimu wanayoidai serikali yatalipwa
kwa awamu iwapo uhakiki utakamilika kwa sasa wanatarajia kulipa kiasi cha
shilingi bilioni 7 kwa walimu 70100 watalipwa Agosti mwaka huu.
“Katika kufanya uhakiki wa madai ya walimu ikiwemo
malimbikizo ya mishara,posho za kufundishia,uhamisho tuligundua kuwa wako
baadhi ya watu walifanya udanganyifu lakini sasa tunamalizia kufanya uhakiki
ili fedha hizo zilipwe” Alisema Kikwete
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Alhaji Yahaya
Msulya amemtaka Raisi Kikwete kushughulikia suala la posho ya kufundishia kwa
walimu kwani walimu ni kundi linalofanya kazi kwa muda mrefu kuliko watumishi
wengine wa serikali.
“Mwalimu anaingia shuleni saa 1:30 asubuhi anatoka saa 3:00
mda huo anatakiwa kusahihisha kazi za wanafunzi na kuandaa masomo ya kufundisha
kesho hivyo anatumia muda mwingi sana katika kazi ni vyema serikali
ikaliangalia suala hili” Alisema Katibu huyo
Katibu huyo ameupongeza uamuzi wa serikali kutoa bure elimu
ya msingi na sekondari ambao utawasaidia watoto wengi hasa waliotoka kwenye
familia zenye kipato cha chini.
No comments:
Post a Comment