Mhe.
Charles Kitwanga ( Mb) Naibu Waziri, Nishati na Madini akizungumzia
namna Tanzania inavyotekeleza Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote
(SE4All) wakati wa Mkutano wa siku Mbili wa Mawaziri wa Sekta ya
Nishani, uliofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Wataalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na Naibu Waziri
katika mkutano huu muhimu uliojadili kwa kina nafasi na umuhimu wa
nishati endelevu kwa wote katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo
endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji wa
mazingira.
Mhe.
Kitwanga akiteta jambo na Mwakilishi wa Bank ya Maendeleo kwaajili ya
Afrika AfDB muda mfupi mara baada ya Naibu Waziri kuzungumza ,
mkutano huu wa SE4All, pamoja na Mawaziri wa sekta husika
umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa vyombo vya
fedha kama vile Bank ya Dunia, AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia
wanamziki maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa
wakichagiza na kuwekeza katika nishati endelevu.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Ngosi Mwihava
akiwasilisha Action Agenda of Tanzania kuhusu SE4All katika moja ya
mikutano iliyofanyika hapa jijini New York.
Kaimu
Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava akiwa na wataalamu wake na
wataalamu washauri wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of
Tanzania.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inaamini kwamba, utekelezaji wa mipango
na malengo ya mbalimbali ya maendeleo hayataweza kupatika au
kufikiwa kwa haraka pasi na uwepo wa nishati endelevu na kwa wote.
Ni
kutokana na kulitambua hilo, Tanzania imejikita kikamilifu katika
kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za
kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja
na kuongeza maradufu kiwango cha uboreshaji na ufanisi wa nishati
mbadala ili kuchagiza maendeleo.
Hayo
yameelezwa siku ya Alhamisi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Mhe. Charles Kitwanga ( Mb), wakati akizungumza katika siku ya pili ya
majadiliano ya mawaziri wanaohusika na sekta ya nishati ambapo kila
waziri aliyehudhuria mkutano huo alipata fura ya kuelezea na kutoa
ahadi ya namna inavyotekeleza mkakati wa nishati endelevu wa wote
(SE4All).
Mhe.
Kitwanga na ujumbe wake unaowashirikisha wataalamu mbalimbali kutoka
Wizara ya Nishati na Madini akiwano Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi
Mwihava wameshiriki kikamilifu katika mkutano huu ulioitishwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo tangu ulipoanza
mapema wiki hii, washiriki wamekuwa wakijadili mada mbali mbali
zinazohusiana na masuala ya nishati, uwekezaji na mchango wake
katika eneo zima la utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
“
Tanzania inaamini kwamba hakuna ajenda za maendeleo zinazoweza
kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wa nishati ya uhakika” akasema
Naibu Waziri
Na
kuongeza kuwa, mkakati wa nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu
katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali inayohitajika
ili kufika malengo ya kitaifa ya nishati endelevu kwa wote kufikia
mwaka 2034 kama inayoainishwa katika mkakati huo.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania ilipitisha mkakati
wa SE4All mwaka 2012 na kufuatiwa na mchakato wa kufanya tathmini
ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea kutoa taarifa ya tathmini
mwaka 2013.
Baada
ya tathmini hiyo ilifuatia misaada kutoka SE4All kwaajili ya Afrika
iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na nchi ( Country Action Agenda)
kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa
Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP).
Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga, taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa udhibitisho mwezi Agosti, 2015.
Aidha
maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji umeanza na utalenga katika
kuangalia mahitaji ya haraka ili kuwezesha mpango huo kuanza
kutekelezwa.
Mkutano kuhusu Nishati Endelevu kwa wote (SE4All) umefungwa jana ( Alhamis).
No comments:
Post a Comment