Afisa
Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard
Mwafongo akiwasilishaji kwa Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko
la Thamani ya mwaka 2014 ambapo alisema kuwa moja kati ya sababu ya
kuandaa sheria hiyo ni kuongeza pato la taifa kupitia makusanyo
mbalimbali wakati wa kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali leo jijini
Dar es salaam.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akijibu hoja
mbalimbali kuhusu Sheria Mpya ya Ongezeko la Thamani toka kwa wadau
waliohudhuria mkutano huo na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano
kuelekea upatikanaji wa sheria hiyo na hatimaye kuwezesha kuinua uchumi
wa nchi.
Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akichangia kwenye moja ya maeneo ya
Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa
mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili maboresho ya sheria
hiyo.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba
kuendelea kutoa ushirikiano kuelekea upatikanaji wa Sheria hiyo
iliyoweza kutumika popote duniani hasa kwenye nchi zinazoendelea
itayowezesha ukusanyaji dhabiti wa Kodi na hatimaye kuchangia maendeleo
ya nchi.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akibadilishana
mawazo na baadhi ya washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Leo Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wadau wakichangia kuhusu Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Kodi
Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard
Mwafongo alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya
ongezeko la Thamani ya mwaka 2014
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
No comments:
Post a Comment