Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) Ezekiah Oluoch akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu
wa chama hicho kitaifa utakaofanyika Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho
utakaofanyika Mei 25 mpaka 28 katika ukumbi wa mikutano wa Ngurudoto,katika
mkutano wake na waandishi wa habari jana uliofanyika katika ofisi za mkoa za
chama hicho,kushoto ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said. Picha na Ferdinand
Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa May 28 mwaka
huu ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 5 pamoja na kutetea maslahi ya
walimu.
Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho Ezekiah Oluoch amesema kuwa nafasi zinazogombaniwa ni
Mwenyekiti wa chama,Katibu,Naibu Katibu mkuu pamoja na Mhazini wa chama hicho.
Ezekiah
alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho Mkoa wa Arusha kuwa hadi sasa
wana jumla ya wanachama 452 wamejitokeza
kugombea nafasi hizo na nafasi nyingine
ikiwamo Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu
,na kitengo cha Walimu wanawake.
“Wagombea ni
wengi na nafasi ni chache tumeona tuache hivyo maana yake tukizuia idadi
tutakua tumeminya demokrasia” Alisema Ezekiah
Ezekiah
amesema kuwa jumla ya walimu 1000 wanatarajia
kushiriki uchaguzi huo wa kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Mkoa wa Arusha (CWT)
Jevin Buruya amesema kuwa wamejiandaa
vyema kwa ajili ya uchaguzi huo hivyo amewataka walimu wajitokeze kwa wingi
katika uchaguzi huo.
Jevin
amesema kuwa Chama cha Walimu Tanzania
kitafanya mkutano mkuu utakaoanza May 25 hadi 28 ambapo agenda kuu ni Uchaguzi
Mkuu,Mkutano huo unatajwa kuwa Mkutano wa Mwisho wa Raisi Kikwete kuwahutubuia
walimu .
No comments:
Post a Comment