Kituo
cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I
kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia
Septemba mwaka huu.
Hayo
yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini
(Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo
la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango
walipotembelea mradi huo.
“Kazi
zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za
kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV
132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi
Jilima.
Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.
Naibu
Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri,
alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake
katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda
na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani
na nje.
“Katika
miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika
uchumi wa viwanda hivyo ni vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili
kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka
2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.
Ili
kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo
mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.
Meneja
Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi
Simon Jilima (kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi
kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani
ni Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert Masatu na Ndg. Aloce
Shayo, kwa mfuatano.
Meneja
Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi
Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya
Mipango, Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi
II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi.
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu.
No comments:
Post a Comment