Waziri
wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini
Dodoma kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei
15,2015.
Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini
Dodoma kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei
15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga
kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa
wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato
cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la
Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na
mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa
kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo
zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati
wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
Waziri
wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha
elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu
yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya
kilele cha Wiki ya Elimu kitaifa iliyofanyika mjini Dodoma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wanafunzi Maria Sagasii na Neema
Harry kutoka Shule ya msingi ya Ignatius ya mjini Dodoma wakionyesha
viungo vya ndani vya mwili wa binadamu somo la Biolojia katia banda la
maonyesho katika Uwanja wa michezi wa Jamhuri wa mjini Dodoma wakati wa
kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu leo.
Baadhi
ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria
sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja
wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .PICHA ZA FREDDY MARO,
IKULU.
No comments:
Post a Comment