Uchumi Wetu : Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Akutana na Joly wa (IMF) , Larose wa Benki ya Dunia - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 23 April 2015

Uchumi Wetu : Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Akutana na Joly wa (IMF) , Larose wa Benki ya Dunia

 Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly  (wa katikati mwenye Tai ya rangi ya chungwa)  akiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa na  ujumbe kutoka Tanzania( hawapo kwenye picha)mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile wakiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile  na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akitoa ufafanuzi na majibu kwaswali aliloulizwa na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  wakijadiliana juu ya kukubaliana kuto kukubaliana kwa baadhi ya sheria za (IMF) na Bw. Nikoloz Gigineishvili ambaye ni Mchimi  mwandamizi wa Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose ofisini kwake wakiwa mjini Washington DC.Walio ambatana na Mhe. Waziri  kutoka kushoto ni Bw. Beda Shallanda Kamishina wa Sera,Bw.Ngosha Said Magonya Kamishina wa Fedha za nje na Bw. John Cheyo Kamishina wa Bajeti na wa pembeni ni mfanyakazi wa Benki ya Dunia.
 
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose ofisini kwake mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose wakiagana mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile , Bw. Beda Shallanda Kamishina wa Sera na Bw. Paul  Mwafongo ambaye ni Afisa katika ubalozi wa Tanzania na kutoka kushoto ni Bw.Ngosha Said Magonya Kamishina wa Fedha za nje Bw. John Cheyo Kamishina wa Bajeti na wa pembeni ni mfanyakazi wa Benki ya Dunia.

Picha zote na Ingiahedi Mduma- Washington DC.

No comments:

Post a Comment