Mfanyabiashara
maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda
vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono
kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata
ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari
yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye
kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.PICHA ZOTE
NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Alhaji
Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha
Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza
kujenga bbandari hiyo mapema mwaka huu.
Msafara wa Alhaji Dangote ukitoka eneo atakalojenga bandari katika Kijiji cha Mgao
Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Dangote akilakiwa na Esther Baruti
Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote
Alhaji
Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto)
Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk, Majanbu
Alhaji Dangote akizungumza na Esther Batuti
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa
wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote
eneo la ujenzi wa Bandari
Alhaji
Dangote akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kijiji cha
Mgfao kukagua eneo la ujenzi wa Bandari pamoja na kiwanja alichopewa na
wanakijiji kujenga makazi yake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho,
Abdulrahman Shaa
No comments:
Post a Comment