Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati
akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa
Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi
wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano
ya Baharini { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar
Ocean View.
Afisa
Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini wa
Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza Bwana Simon Tucker akielezea
umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya
usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya
Baharini hapa Zanzibar.
Balozi
Seif akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa
pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia
ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } ya Nchini Uingereza na
watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa
ni sehemu ya Dunia hii inahitaji kuendelea kuwa salama na tulivu
kutokana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe zote.
Alisema
mfumo wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali
Duniani uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari yenye kutoa utajiri
mkubwa kwa asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa kutumika ili kuondoa
shaka katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo
mbali mbali hapa Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati
ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya
mawasiliano ya Baharini { SRT } ya Nchini Uingereza na watendaji wa
Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar Ocean View Kilimani
Mjini Zanzibar.
Alisema
yapo matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi
kuibuka na kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo yalikuwa
yakitekelezwa na maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano uliokuwepo
wakati huo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa
kisasa waTeknolojia ya mawasiliano ya Baharini unaotumiwa na Kampuni
ya { SRT } ya Nchini Uingereza katika Mataifa mbali mbali
Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la uharamia katika maeneo ya
Baharini.
Akiwasilisha
mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye Mkutano huo
Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini
wa { SRT } Bwana Simon Tucker alisema kifaa maalum cha Mawasiliano
huwekwa kwenye chombo cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za
mawasiliano.
Bw.
Simon alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au
hata meli za uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya
mawasiliano kwa zidi ya meli 40.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment