Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa
harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha
kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha
za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao
ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
|
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo. |
|
Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga |
|
Wajumbe wa Imetosha |
Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za
Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa
kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na
unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina
mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo
mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.
|
Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo |
|
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha |
Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba
wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula
mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa”
alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga
kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis
alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho
kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa
ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284
wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo
chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa
kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.
Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho
|
Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watoto wimbo waupenda wa Clap your hands! |
|
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga |
|
Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho |
|
Katibu wa Imetosha ambaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali |
Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira
No comments:
Post a Comment