Wanawake Wanaweza : Mama Salma Kikwete Mgeni Rasmi Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Mkoani Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 9 March 2015

Wanawake Wanaweza : Mama Salma Kikwete Mgeni Rasmi Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Mkoani Dar es Salaam


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar es Salaam terehe 8.3.2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuyapokea maandamano ya akina mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015.
Wafanyakazi akina mama kutoka Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakifuatiwa na Jeshi la zimamoto.
Wafanyakazi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC, wakifuatiwa na wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari leo pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nao wakipita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi.
Wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakipita huku wakishangilia kwa furaha mbele ya mgeni rasmi.Kwa Picha Zaidi BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment