Matukio : Waziri Nyalandu Awapa Milioni 100 Wafanyabiashara wa Maduka ya Vinyago, Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 20 March 2015

Matukio : Waziri Nyalandu Awapa Milioni 100 Wafanyabiashara wa Maduka ya Vinyago, Jijini Arusha

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la vinyago jijini Arusha wakiandaa bidhaa kwa ajili ya kuuza kwa watalii wanaotembelea soko hilo mara kwa mara kujipatia vinyago hivyo wanaporudi makwao kama walivyokutwa na blog hii mapema leo kabla ya waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa Lazaro Nyalandu aliyefanya ziara ya ghafla ili kujua maendeleo yao
Waziri wa maliasili na Utalii mheshimiwa Lazaro Nyalandu kushoto akiwa na katibu mkuu wa wizara hiyo Dokta Adelhelm Meru akipewa maelezo na mwenyekiti wa soko la vinyago (hayupo pichaniI) juu ya ujenzi wa soko la vinyago (Ambalo liliungua Moto lote) maarufu kwa jina la Mount Meru curious mapema leo.  soko hilo liliungua na kusababisha hasara kubwa kwa wajasiriamali hao wapatao 250 na kutoa ajira kwa zaidi ya watu 500 
Waziri Nyalalndu na katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dk. Meru wakistaajabia ujenzi wa soko hilo la kisasa ambapo waziri huyo aliwapa msaada wa shilingi millioni mia moja kupitia shirika la hifadhi za taifa nchini TANAPA
wafanyabiashara hao wakimsikiliza kwa makini waziri wa maliasili na utalii nchini Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza nao mapema leo katika soko la vinyago la mount mertu curious lililokuwa limeungua hivi karibuni
Wafanyabiashara hao wa soko la vinyago lililopo karibu na ofisi ya ccm wilaya Arusha wakishangilia mara baada ya Waziri Nyalandu alipowapa msaada wa juml;a ya shilingi milioni mia moja na kuwaahidi kuwa serikali yake na wizarara yake itahakikisha kuwa tozo ya kodi ya vinyago itafutwa ili kuhakikisha soko la vinyago linakuwa la uhakika na kutoa ajira kwa familia zaidi ya mia tano.

No comments:

Post a Comment