Mwenyekiti
wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu huria kituo cha Manyara, Mwalimu
Pasian Siay akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, iliyofanyika jana mjini Babati.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera, akizungumza jana mjini Babati
wakati wa kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly
Mbwette, (kushoto) na aliyepo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin
Meela.
Mkurugenzi
wa chuo kikuu huria kituo cha Manyara Dk Joseph magali (kushoto)
akimpongeza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini (OUT) Profesa Tolly
Mbwette (kulia) baada ya kuvikwa vazi la jadi la jamii ya watu wa mkoa
wa Manyara jana, kwenye hafla ya kumuaga profesa huyo ambaye
amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vyuo vikuu vya Afrika nzima.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini (OUT) Profesa Tolly Mbwette (kulia)
akikabidhiwa cheti cha heshima jana na Mkurugenzi wa chuo kikuu huria
kituo cha Manyara kwenye hafla ya kumuaga profesa huyo ambaye
amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vyuo vikuu vya Afrika nzima.
Mkuu
wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela, akizungumza kwenye
hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly
Mbwette, iliyofanyika jana mjini Babati.
Baadhi
ya wakazi wa Mjini Babati Mkoani Manyara waliohudhuria hafla ya kumuaga
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, alipoagwa
jana kwenye kituo cha chuo hicho mjini Babati.
No comments:
Post a Comment