Maisha Yetu: Watoto Waishio Kwenye Mazingira Magumu Kujengewa Sehemu ya Kulala (Hostel) Jijini, Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 3 March 2015

Maisha Yetu: Watoto Waishio Kwenye Mazingira Magumu Kujengewa Sehemu ya Kulala (Hostel) Jijini, Arusha


Baadhi ya Watoto wa mitaani waishio jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao.
Kikundi cha ngoma cha watoto wa mitaani wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao.

Na Ferdinand Shayo wa Blogu ya Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Watoto wa mitaani wanaoishi  jijini Arusha katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.

Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wa mitaani jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto wa mitaani kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Sawale alisema kuwa iwapo watoto wa mitaani watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .

“Watoto wa mitaani tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya” Alisema Sawale

Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa  Panju  alijitolea kuwasaidia watoto wa mitaani kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa watoto hao ili waweze kupata mahitaji muhimu  ,Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wa mitaani wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa .

“Maisha ya baadae yanawategemea watoto wa sasa ambao ndio sisi watoto wa mitaani juhudi zikiimarishwa wanaweza kuchangia maendeleo kwa taifa letu” Alisema Hassan

No comments:

Post a Comment