Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya gari la wagonjwa (ambulance)
kwa Meya wa Mji wa Masasi Mheshimiwa Andrew Mtumsha kwenye sherehe
iliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi tarehe 19.3.2015.
Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa
Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara ni Ndugu Halima Dendegu.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na
serikali kuangalia sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa kwenye hospitali ya Mkomaindo.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiagana na wananchi mbalimbali kwa kuwapungia
mikono baada ya kukamilisha zoezi la kukabidhi gari la wagonjwa kwenye
hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa wauguzi katika
hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, mara baada ya kuwasili
hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatembelea wagonjwa tarehe 19.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimwelekeza Bibi Zauda Amuli,18, mkazi wa Mtaa
wa Moroco namna ya kumnyonyesha mtoto wake mchanga aliyezaliwa tarehe
17.3.2015 katika hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimchukua mtoto mchanga kutoka kwa mama yake
Bibi Malisela Amandus, 24, anayeishi mtaa wa Silabu huko Masasi wakati
Mama Salma alipotembelea hopitalini hapo kuwajulia hali wagonjwa tarehe
19.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Ndugu
Halima Dendegu (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkomaindo
Dkt. Musa Rashid (kulia) wakitembelea maeneo mbalimbali ya hospitali
hiyo.
Mama
Salma Kikwete, Mke wa Rais akiwasalimia wazee wa Mji wa Masasi wakati
alipowasili kwenye eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi kwa ajili
ya kukabidhi gari la wagonjwa kwenye hospitali ya Wilaya, Mkomaindo,
tarehe 19.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwasslimia wanafunzi waliofika kwenye sherehe
ya kukabidhi gari la wagonjwa (ambulance) kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Masasi, Mkomaindo, tarehe 19.3.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment