Raisi wa Mahakama ya
Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani Akihutubia mkutano
wa Haki za binadamu uliofanyika jana jijini Arusha lengo la kuimarisha
haki za binadamu na kushirikisha taasisi binafsi na za serikali katika
kuisaidia Mahakama hiyo .Picha
na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog - Arusha.
Raisi wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu
Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa lugha ya Kiswahili itaanza kutumika katika
mahakama hiyo ili kuwawezesha watu kusoma na kuelewa taarifa muhimu
zinazotolewa zitakazowawezesha kujua na
kuimarisha haki hizo za msingi kwa kila mmoja
.
Jaji
Agustino Ramadhani amesema kuwa lugha ya Kiswahili inazungumzwa na nchi nyingi
barani Afrika hivyo umefika wakati wa kubadilisha taarifa na nyaraka mbali
mbali kutoka lugha za kigeni na kuwa
katika Kiswahili ili kukuza uelewa wa watu juu ya haki za binadamu.
Raisi huyo
ameeleza hayo katika mkutano wa haki za binadamu ulioandaliwa na Mahakama hiyo
kwa kushirikiana na Mashirika na taasisi binafsi zinazojihusisha na haki za
binadamu uliofanyika jijini Arusha jana,Ramadhani amesema kuwa mashirika
binafsi yana nafasi kubwa ya kutoa elimu
kwa wananchi na kuhamasisha uzingatiaji wa haki hizo.
Mwenyekiti
wa Mashirika binafsi yanayotetea haki za binadamu na kufanya kazi kuisaidia
mahakama hiyo George Kisoro amesema kuwa
suala la kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya Makosa ya jinai kwa mujibu wa
mkataba wa Malabo unaojulikana kama
Malabo Protocol na kupitishwa Juni 2014 bado una kasoro mojawapo ni kuwepo kwa
kifungu ambacho hakiruhusu rahisi kushitakiwa akiwa katika kipindi cha uongozi
wake.
“Kifungu
hichi kitawafanya viongozi wa Afrika kung`ang`ania madaraka kwa kuogopa kuwa
iwapo wakiachia madaraka watashitakiwa katika mahakama hiyo kwa upande mwingine
ina madhaifu” Alisema George
George
alisema kuwa kutokana na Viongozi wa Afrika kutorishiwa na mwenendo wa Mahakama
ya kimataifa ya makosa ya jinai iliyoko
the Heague walipendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Afrika ya makosa ya
jinai itakayoendesha makosa ya jinai yanayowakabili viongozi.
Anaeleza
kuwa kwa sasa hali ya haki za binadamu kwa bara la Afrika bado ni mbaya hasa
katika maeneo yenye vita kama nchini Congo na Sudan ambako vitendo vya kikatili
na unyanyasaji wanafanyiwa wanawake na watoto ikiwemo ubakaji,kukatwa viungo
vya mwili,vipigo vikali .Katika maeneo
hayo kuuana imekua ni utamaduni wa kudumu suala ambalo si zuri.
No comments:
Post a Comment