Habari na Maisha : Kipindi cha Maskani ya Times FM Waadhimisha siku ya Wanawake kwa Kutoa Msaada katika Hospitali ya Mwananyamala, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 10 March 2015

Habari na Maisha : Kipindi cha Maskani ya Times FM Waadhimisha siku ya Wanawake kwa Kutoa Msaada katika Hospitali ya Mwananyamala, Jijini Dar


Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk, Sophinias Ngonyani (kulia) mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote. Wanaoshuhudia ni Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi wa Mazinat Bridal Maza Sinare. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni 'Uwezeshaji Wanawake, Tekeleza Wakati ni Sasa'. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Wakifurahia msaada.
Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Stanslaus Lambat (wa kwanza kulia) akiendelea kurusha matangazo live toka eneo la tukio.
Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Sandra Temu akiongea machache mara baada ya makabidhiano kufanyika.
Viongozi wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa alisema kuwa Times Kupitia kipindi cha Maskani walifika kuungana na watu wote duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Kila mmoja anatambua changamoto zinazoikabili sekta ya afya hapa nchini hivyo wa kutambua hilo wameamua kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuchangia mashuka 200 kwa ajili ya wodi ya akinamama na watoto kwenye hospitali ya Mwananyamala.

Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azan akitoa shukrani kwa uongozi wa Times Fm kwa kujitoa kutoa msaada katika jimbo lake.
 Mbunge waa Kinondoni Mhe.Idd Azzan akiongea na mtangazaji wa Kipindi cha Maskani cha Times Fm Sandra Temu mara baada ya kufika katika hospitali kuungana nao kutoa msaada wa mashuka kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Mtayarishaji wa Kipindi Cha Maskani Zhora Zuri (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo machache mara baada ya kuingia katika hospitali ya Mwananyamala kutoa msaada. Pembeni ni Watangazaji wa kipindi hicho Sadra Temu, Stanslaus Lambat (mwenye shati nyeupe) na rafiki yao mwenye tisheti nyeusi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk, Sophinias Ngonyani (katikati) akitoa  maelezo kwa Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa Machi 8, duniani kote.
Wakunga wa hospitali ya Mwananyamala wakiwa wameshika mashuka mara baada ya kukabidhiwa.
Umati wa Watu waliofika kushuhudia makabidhiano hayo.
Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa wakitandika kitanda mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote.
 Mmoja ya akinamama akitoa shukrani kwa uongozi wa Times Fm kwa masaada waliotoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa akiongea na wafanyakazi wa Maznat Bridal mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote.
 Mtayarishaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Zhora Zuri akitoa maelekezo kwa Mtangazaji wa Kipindi hicho Sandara Temu.
Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan akiongea na Mtayarishaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Zhora Zuri.
Timu ya Maznat Bridal ikiwakilisha.

No comments:

Post a Comment