Nishati na Madini : Sekta ya Madini inakabiliwa na changamoto za Uhaba wa Waalimu wa Ukataji Madini - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

4 Feb 2015

Nishati na Madini : Sekta ya Madini inakabiliwa na changamoto za Uhaba wa Waalimu wa Ukataji Madini


SAM_0921 Mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa Shanyangi akiongea na waandishi wa habari hivikaribuni kuhusu namna kituo hicho kinavyotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito
SAM_0919Mwalimu msaidizi wa chuo hicho Bw.Jamal Dallos akiwa anaendelea na shughuli ya ukataji madini
SAM_0897Lilian Petro akikata madini kwaajili ya kutengeneza pete,mkufu ,jiwe hilo ni aina ya Quartz shape Oval
SAM_0898Grace Charles akiendelea na ukataji wa madini
SAM_0899Kulia ni Gladness John pamoja na Loveness Marteen wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji
SAM_0900Magret Joseph akiwa anaangalia kwa makini namna alivyokuwa akikata jiwe kwa kutumia mashine maalum
SAM_0912Loveness Marteen anachukua fursa hiyo kuwataka wanawake wengine kujitokeza katika fani hiyo ya ukataji madini kwa kuwa hata wanawake wanaweza kufanya shughuli hizo kama wanaume
SAM_0917Aina mbalimbali ya madini kabla ya kukatwa
SAM_0918
Baada ya kukatwa na mashine muonekano huwa hivi
SAM_0908Wanafunzi wakiwa darasani wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji madini . Picha na Pamela Mollel wa Jamii Blog

Sekta ya madini nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu na wataalamu wa kufundisha ukataji wa vito vya madini hali inayosababisha kuuzwa kwa madini ghafi nje ya nchi na kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini na pesa nyingi kwenda nje Hayo yameelezwa leo na mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa Shanyangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika kituo hicho kina kinachotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito wakati wa mahojiano maalum na waandishi wahabari chuoni hapo ambapo wameanza kutoa mafunzo ngazi ya cheti kwa wahitimu 15 wakike ambapo chuo kipo katika halmashauri ya manispaa ya jiji la arusha.
Alieleza kuwa hivi sasa madini ghafi yanauzwa sana nje ya nchi kwa bei ya chini lakini kama wangeweza kuuza madini hayo yakiwa yameongezwa thaman na kuuzwa kwa bei ghali na kuwezesha fedha za kigen kubaki nchini na kuongeza pato la taifa .
Bw,Shanyangi aliongeza kuwa hivi sasa wameanza kuwafundisha kozi ya miezi 6 kwa wanafunzi 15 wakike ambapo wanafadhiliwa na Arusha women foundation fund iliyoko mjini ikiwa na lengo la kuwasaidia mabinti ili kuweza kusaidia sekta ya madini na kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalamu wa ukataji madini nchini. Hata hivyo kituo hicho kinatarajia kuongeza wanafunzi mpaka kufikia 60 ili kuweza kuongeza ufanisi na kuweza kuboresha sekta hiyo ya madini ili kuweza kuongeza wataalamu ,pia wanamkakati wa kuweza kusomesha walimu wazawa ili kuweza kukidhi nakuwa na walimu na kupunguza gharama za kuchukua mwalimu kutoka nje yanchi ambapo hivi sasa wamemuajiri raia kutoka Sri lanka hali ambayo wanatumia gharama kubwa kumlipa mtaalamu huyo toka nje ya nchi.
BwShanyangi aliwataka wadaumbalimbali nchini pamoja na wawekezaji wawekeze katikak kufundisha wataalamu wazawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakataji na wataalamu nchini.
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi billion 1.2na mashine mbalimbali za kituoni hapo zimegharimu zaidi ya milioni 450 za ukataji na kusafisha madini hayo Kwa upande wake mwanafunzi katika chuo hicho Bi.Joice Patrick alisema kuwa kupitia mafunzo hayo ya ukataji wa madini na ung’arishaji itawasaidia katika swala zima la ajira huku akiwataka wanawake kuchangamkia fursa hiyo “Ni fursa sasa kwa wanawake kujitokeza katika kazi hii na waione kama kazi zingine na si kuwaachia wanaume tu “alisema Joice

No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633