Matukio: Tume ya Utumishi wa Mahakama Yaendesha Mafunzo ya Siku Mbili kwa Kamati za Maadili za Mikoa ya Rukwa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 12 February 2015

demo-image

Matukio: Tume ya Utumishi wa Mahakama Yaendesha Mafunzo ya Siku Mbili kwa Kamati za Maadili za Mikoa ya Rukwa


IMG_4687
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015. Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi. 
IMG_4723
Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji Ferdinand Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12 Februari na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).
IMG_4703
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi akitoa shukurani za Mikoa ya Rukwa na Katavi kwa kuletewa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa Kamati za maadili za Mikoa hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku.
IMG_4676
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Iddi Kimanta (wa kwanza) na Katibu Tawala Wilaya Kalambo Bi Mapinduzi Severian ambao ni Wajumbe wa Kamati ya maadili Mkoa wa Rukwa wakifuatilia mafunzo hayo.
IMG_4684
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za maadili Mkoa wa Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
IMG_4686
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa kwanza) na wajumbe wengine wa Kamati za Maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
IMG_4694
Mafunzo yakiwa yanaendelea.
IMG_4705
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *