Siasa Zetu : Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yakutana na Viongozi wa Siasa, Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 12 February 2015

demo-image

Siasa Zetu : Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yakutana na Viongozi wa Siasa, Jijini Dar es Salaam

DSC_0102
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
DSC_0091
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
DSC_0249
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
DSC_0111
Mwenyekiti wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo.
DSC_0122
Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.
DSC_0193
Eeehh....bwanaaaaa upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na Emmanuel Massaka

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *