Uongozi Wetu : Rais Mstaafu wa Botswana na Mhe. Festus Mogae Atembelea Taasisi ya Uongozi , Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 15 January 2015

Uongozi Wetu : Rais Mstaafu wa Botswana na Mhe. Festus Mogae Atembelea Taasisi ya Uongozi , Jijini Dar es Salaam


Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kushoto) akipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja pale kiongozi huyo mstaafu alipotembelea ofisi hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Rais jana Masaki, jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za UONGOZI Institute pale alipofika kwenye taasisi hiyo kufahamu zaidi kuhusu maendeleo yake. Anayeshuhudia kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja na Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa taasisi hiyo Bw. Dennis Rweyemamu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja (wa pili kushoto) akimuelezea Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kulia) kuhusu mradi wa ujenzi wa taasisi ya mafunzo ya UONGOZI Institute unaoendelea katika mji wa Bagamoyo, Pwani. Kutoka kulia ni Dr. Linda Ezekiel Mkurugenzi wa Sekta za Kijamii kutoka Presidential Delivery Bureau (PDB) na Mkuu wa Sera na Utafiti wa UONGOZI Institute Bw. Dennis Rweyemamu.
Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae pia alipata wasaa wa kuzungumza na wafanyakazi wa UONGOZI Institute, kuelezea kuhusu uzoefu wake katika uongozi, utumishi wa umma, pamoja na maono yake kwa bara la Afrika na watu wake.
Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae akizungumza na wafanyakazi wa UONGOZI Institute (hawapo pichani) taasisi inayojishughulisha na utoaji mafunzo ya uongozi kwa viongozi serikalini pamoja na utafiti na ushauri wa kisera unaoweza kuleta maendeleo endelevu nchini. Pembeni yake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja.
Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (aliyeketi kulia) na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja (aliyeketi kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UONGOZI Institute jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment